Lugha Nyingine
Maonyesho ya biashara na utalii ya Namibia yachochea ukuaji
(CRI Online) Novemba 03, 2025
Kampuni za Namibia zimetumia Maonyesho ya Biashara na Utalii ya Erongo yaliyofanyika katika Kituo cha Kiraia cha Manispaa ya Walvis Bay, nchini humo kuchochea ukuaji wa biashara na uvumbuzi.
Maonyesho hayo ambayo ni ya 17, hufanyika kila mwaka katika mji wa pwani wa Walvis Bay, ambako washiriki zaidi ya 160, wakiwemo wamiliki wa kampuni, biashara, na wadau kutoka sekta za hoteli, utalii, na viwanda vya magari wanaonyesha bidhaa na huduma zao.
Pia bidhaa za jadi na kitamaduni kama sanaa za mikono na vyakula pia vinachukua nafasi kubwa katika maonyesho hayo.
Maonyesho hayo yalifanyika kuanzia Oktoba 28 hadi Novemba 1 chini ya kaulimbiu ya "Kuchochea Uvumbuzi na Kuhimiza Uchumi wa Bluu na Vichocheo vya Kuzalisha Ajira vya Namibia".
(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



