Lugha Nyingine
Rais Xi na mwenzake Lalabalavu wa Fiji watumiana salamu za pongezi juu ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhusiano
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Fiji Ratu Naiqama Lalabalavu wametumiana salama za pongezi kwa maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Fiji, katika salamu zake alizotuma jana Jumatano, Rais Xi amesema kuwa Fiji ni nchi ya kwanza ya visiwa vya Bahari ya Pasifiki kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Jamhuri ya Watu wa China.
Ameongeza kuwa tangu kuanzishwa kwa uhusiano huo wa kidiplomasia miaka 50 iliyopita, nchi hizo mbili siku zote zinaheshimiana, kutendeana kwa usawa na kutafuta ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote, na kuungana mkono katika njia ya maendeleo ya kila nchi inayolingana na hali halisi ya nchi yao, bila kujali mabadiliko katika hali ya kimataifa.
"Katika miaka ya hivi karibuni, pande zote mbili zimepata matokeo yenye matunda mazuri katika kusukuma mbele kwa pamoja ushirikiano wa sifa bora wa ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, zikileta manufaa kwa watu wao, na kufanya urafiki kati ya nchi hizo bili kuwa wa dhati zaidi," Rais Xi amesema.
Amesisitiza kwamba anaweka umuhimu mkubwa kwenye maendeleo ya uhusiano kati ya China na Fiji na anapenda kushirikiana na Rais Lalabalavu kuchukua maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kuwa fursa ya kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa, kupanua ushirikiano katika sekta mbalimbali, na kuinua uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Fiji kwenye kiwango cha juu zaidi.
Kwa upande wake, Rais Lalabalavu amesema kwamba maadhimisho hayo ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Fiji na China ni hatua muhimu katika uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
"Kwenye msingi wa matarajio ya pamoja ya kuheshimiana, maslahi ya pamoja na amani na ustawi, nchi hizo mbili zimeanzisha ushirikiano wa kimkakati wa pande zote," amesema, akiongeza kuwa ushirikiano huo unaendelea kupanuka, ukitoa mchango muhimu kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za kikanda na kimataifa.
Amesema kuwa, maendeleo ya uhusiano kati ya Fiji na China yataendelezwa kwa kina zaidi, kuwa na nguvu hai zaidi na hata kuwa na matarajio mapana zaidi.
Siku hiyo ya jana Jumatano, Waziri Mkuu wa China Li Qiang na mwenzake wa Fiji Sitiveni Rabuka walitumiana salamu za pongezi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



