Kenya yaipongeza kampuni ya Huawei ya China kwa kuendeleza suluhu za nishati endelevu

(CRI Online) Novemba 06, 2025

Kenya imeipongeza kampuni ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ya Huawei ya China kwa mchango wake wa kuendeleza suluhu za nishati endelevu nchini humo.

Waziri wa Nishati na Mafuta wa Kenya Bw. James Opiyo Wandayi, amesema teknolojia za hali ya juu za kidijitali, gridi mahiri ya umeme, na mifumo ya usimamizi wa nishati kutoka Huawei vinaharakisha mageuzi ya miundombinu ya nishati ya Kenya, na kuifanya iwe yenye ufanisi, ya uhakika na endelevu zaidi.

Akiongea jana Jumatano kwenye Mkutano wa Nishati wa Huawei Tawi la Kenya, waziri huyo ameipongeza Huawei kwa uongozi wake katika kuchochea mageuzi ya kidijitali ya nishati na pia kwa dhamira yake thabiti ya kuunga mkono maendeleo ya Kenya na Afrika kwa ujumla.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha