ECOWAS yaelezea mshikamano na Nigeria kufuatia madai ya Trump ya mauaji ya Wakristo

(CRI Online) Novemba 06, 2025

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imeyaelezea madai ya hivi karibuni ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kwamba mashambulizi ya kigaidi nchini Nigeria yamekuwa yakilenga Wakristo kuwa ni "ya uwongo na hatari," ikielezea mshikamano wake na nchi hiyo yenye watu wengi zaidi katika eneo hilo.

Katika taarifa iliyotumwa kwa Shirika la Habari la China, Xinhua jana Jumatano mjini Abuja, mji mkuu wa Nigeria, Kamisheni ya ECOWAS imesisitiza kwamba, vurugu zinazohusiana na ugaidi hazibagui kulingana na jinsia, dini, kabila, au umri, ikisema wahusika wa vurugu hizo wanalenga raia wasio na hatia wa madhehebu yote ya kidini, wakiwemo Waislamu, Wakristo, na wafuasi wa imani nyingine.

Huku ikipinga vikali “madai hayo ya uwongo na hatari ambayo yanazidi kuongeza hali ya ukosefu wa usalama katika jamii na kudhoofisha mshikamano wa kijamii katika eneo hilo,” ECOWAS imeihimiza dunia kusimama upande wa nchi za eneo hilo katika vita vyao dhidi ya ugaidi unaolenga jamii zote.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha