Lugha Nyingine
Zambia yarekodi kupungua kwa asilimia 8.2 kwa ukatili wa kijinsia katika robo ya tatu ya mwaka
(CRI Online) Novemba 06, 2025
Polisi nchini Zambia imesema, nchi hiyo imerekodi kupungua kwa matukio ya ukatili unaotokana na jinsia (GBV) kwa asilimia 8.2 katika robo ya tatu ya mwaka 2025, ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho.
Msemaji wa Jeshi la Polisi la Zambia, Rae Hamoonga amesema kupitia taarifa iliyotolewa Jumanne wiki hii kuwa jumla ya matukio 9,899 ya ukatili wa kijinsia yalirekodiwa katika robo ya tatu ya mwaka huu, ikilinganishwa na matukio 10,782 yaliyoshuhudiwa mwaka jana kipindi kama hicho.
Msemaji huyo amesema, kupungua huko kunaonesha mwelekeo chanya wa kupungua kwa ukatili wa kijinsia, na kuakisi ufanisi wa juhudi zinazoendelea za kuelimisha umma na uingiliaji kati wa kijamii.
(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



