Lugha Nyingine
Bandari ya nchi kavu Kaskazini mwa China yashughulikia treni za mizigo za China-Ulaya zaidi ya 15,000 katika miaka mitano
Picha iliyopigwa Septemba 3, 2025 ikionyesha treni ya mizigo ya China-Ulaya ikiingia kwenye bandari ya reli ya Erenhot, Mkoa Unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, Kaskazini mwa China. (Picha na Guo Pengjie/Xinhua)
HOHHOT – Forodha ya Hohhot katika Mkoa Unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, Kaskazini mwa China imesema, katika kipindi cha Mpango wa 14 wa Miaka Mitano wa China (2021-2025), zaidi ya treni 15, 000 za mizigo za China-Ulaya zimepita Bandari ya Erenhot, bandari kubwa zaidi ya nchi kavu kati ya China na Mongolia.
Ikiwa ni bandari pekee ya usafirishaji kwa "ushoroba wa katikati" wa mtandao wa treni za mizigo za China-Ulaya, Bandari ya Nchikavu ya Erenhot sasa inaendesha njia 74 zinazounganisha miji na vituo zaidi ya 140 katika sehemu mbalimbali za Asia na Ulaya.
Forodha hiyo imesema, muundo wa usafirishaji bidhaa za kuuzwa nje umeboreshwa, huku bidhaa zenye thamani ya nyongeza kubwa kama vile magari, mashine na vifaa vya kielektroniki zikichukua asilimia zaidi ya 40 ya bidhaa zote zinazosafirishwa.
Mamlaka za forodha zimeongeza ufanisi kwa kupitia mifumo ya usimamizi ya teknolojia za kisasa.
"Hatua hizi zinahakikisha ongezeko tulivu la treni za mizigo," amesema Li Dawei, ofisa wa forodha katika Bandari ya Erenhot.
Takwimu zilizotolewa zinaonesha kuwa, katika robo tatu za kwanza za mwaka huu, idadi ya treni za mizigo za China-Ulaya zilizoingia na kutoka kwenye bandari hiyo ilifikia 2,904, ikiwa ni ongezeko la asilimia 11.4 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



