Semina ya ngazi ya juu yatoa wito wa kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika ili kuendeleza viwanda Afrika

(CRI Online) Novemba 07, 2025

Semina ya ngazi ya juu iliyofanyika jana Alhamisi mjini Addis Ababa nchini Ethiopia, imetoa wito wa kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya China na Afrika kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya sekta ya viwanda barani Afrika.

Ikiwa na kaulimbiu ya "China Kuunga Mkono Maendeleo ya Viwanda Barani Afrika: Kuhimiza Maendeleo ya Kijani, Yaliyoratibiwa na Endelevu", semina hiyo imeleta pamoja wataalam na watunga sera kutoka China na Afrika, pamoja na wawakilishi kutoka Umoja wa Afrika, mashirika ya Umoja wa Mataifa, taasisi za washauri bingwa na wasomi.

Mkuu wa Ujumbe wa China katika Umoja wa Afrika Balozi Jiang Feng, amepongeza maendeleo ya kiviwanda yaliyopatikana hivi karibuni barani Afrika, kama yanavyojidhihirisha kwa kuanza kufanya kazi kwa Makubaliano ya Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika na mikakati ya maendeleo ya kitaifa barani kote.

Balozi Jiang amesisitiza nia ya China ya kushirikiana na Umoja wa Afrika na nchi za Afrika kwenye utekelezaji wa mpango wa kuunga mkono maendeleo ya viwanda ya Afrika na matokeo ya Mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha