China na Burkina Faso zasherehekea mavuno ya mpunga, zasisitiza ushirikiano wa karibu zaidi wa kilimo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 10, 2025

Picha hii iliyopigwa Novemba 6, 2025 ikionyesha  Sherehe ya kwanza ya Mavuno ya Urafiki kati ya China na Burkina Faso iliyofanyika Boulbi, Mkoa wa Kadiogo, Burkina Faso. (Timu ya China ya msaada wa kiufundi wa kilimo/kupitia Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Novemba 6, 2025 ikionyesha Sherehe ya kwanza ya Mavuno ya Urafiki kati ya China na Burkina Faso iliyofanyika Boulbi, Mkoa wa Kadiogo, Burkina Faso. (Timu ya China ya msaada wa kiufundi wa kilimo/kupitia Xinhua)

OUAGADOUGOU - Sherehe ya kwanza ya Mavuno ya Urafiki kati ya China na Burkina Faso imeanza huko Boulbi, Mkoa wa Kadiogo, likisherehekea hatua muhimu katika ushirikiano wa kilimo kati ya nchi hizo mbili ambapo sherehe hiyo iliyofunguliwa Alhamisi, imevutia maafisa wa China na Burkina Faso, wataalamu wa kilimo, na wakulima wenyeji zaidi ya 100 huko Boulbi, umbali wa kilomita takriban 20 kusini-mashariki mwa mji mkuu, Ouagadougou, ambao pia unakaliwa na kituo cha kielelezo kwa aina mpya za mpunga.

Balozi wa China Zhao Deyong na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo ya Burkina Faso Gaoussou Sanou walifungua hafla hiyo kwa kukata mabegu ya kwanza ya mpunga. Kisha washiriki walitembea mashamba ya kielelezo yanayoonyesha aina 16 mpya za mpunga chotara wa Kichina, wakifuatilia ukuaji mimea na kutathmini mavuno ya msimu wa mvua wa mwaka huu.

Akizungumza kwenye shughuli hiyo, Balozi Zhao amepongeza ushirikiano huo wa kilimo kati ya pande mbili.

"Kilimo ni msingi wa maendeleo ya taifa. China itaendelea kushirikiana kwa karibu na Burkina Faso ili kubadilishana uzoefu, kuzidisha ushirikiano, na kusaidia nchi hiyo kufanikisha kujitosheleza kwa chakula na kufikia kilimo kisasa." amesema.

Kwa upande wake Sanou amesisitiza umuhimu wa ushirikiano huo kwa ajili ya usalama wa chakula wa taifa.

"Aina tatu za mpunga chotara zilizochaguliwa na wataalamu wa China zimeonyesha utendaji bora sana katika majaribio ya kikanda... Ziliidhinishwa kulimwa kote nchini mwaka 2024, aina hizi zina uwezo mkubwa wa kustahimili mabadiliko na mavuno makubwa, zikikamilisha kwa ufanisi aina za kienyeji," Sanou amesema.

Mkulima mwenyeji wa mpunga Issaka Ouedraogo ameeleza furaha yake: "Mavuno ya mwaka huu yamezidi yale yaliyopita. Tumeridhika sana na aina mpya za mpunga. Shukrani kwa kazi ngumu ya wataalamu wa China, na tunatumai China itaendelea kutoa msaada wake, ambao ni muhimu katika kuboresha mavuno na kufikia kujitosheleza kwa chakula."

Burkina Faso imekuwa ikikabiliwa na uhaba wa chakula kwa muda mrefu, huku kilimo kinachotegemea mvua kikiathiriwa na hali mbaya ya hewa, ukame, na mafuriko. Likiwa ni zao la msingi, mpunga ni muhimu kwa usalama wa chakula wa taifa, na serikali imeweka kipaumbele katika maendeleo ya kilimo cha mpunga kwenye Mpango wake wa Kilimo na Uvuvi wa 2023-2025 ili kufikia kujitosheleza.

Tangu uhusiano wa kidiplomasia ulipoanzishwa tena mwaka 2018, timu ya China ya msaada wa kiufundi wa kilimo imeanzisha miradi ya msaada ili kuimarisha usalama wa chakula na maisha ya vijijini nchini Burkina Faso.

Kwa mujibu wa timu hiyo ya China, awamu mbili za kwanza za miradi ya msaada zilisaidia kukuza hekta 2,000 za mpunga wa nyanda za chini na kupanua hekta 30,000 za maeneo mapya ya kilimo. Awamu ya tatu, iliyoanza Machi 2025, inahusisha wataalamu wanane katika kilimo cha mpunga, umwagiliaji, mashine za kilimo, ufugaji mifugo, na uvuvi, ikilenga kukuza mpunga chotara wenye mavuno makubwa, kupunguza umaskini vijijini, na kuanzisha vijiji vya kielelezo na maeneo ya maonyesho ya aina mbalimbali za mpunga.

Picha hii iliyopigwa Novemba 6, 2025 ikionyesha kituo cha kielelezo cha aina mpya za mpunga huko Boulbi, Mkoa wa Kadiogo, Burkina Faso. (Timu ya China ya msaada wa kiufundi wa kilimo/ kupitia Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Novemba 6, 2025 ikionyesha kituo cha kielelezo cha aina mpya za mpunga huko Boulbi, Mkoa wa Kadiogo, Burkina Faso. (Timu ya China ya msaada wa kiufundi wa kilimo/ kupitia Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha