Roboti za China zavutia zaidi kwenye Mkutano wa kilele wa Wavuti mjini Lisbon, Ureno

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 14, 2025

Roboti ya Kampuni ya Roboti ya Unitree ikipeana ishara na washiriki kwenye Mkutano wa kilele wa Wavuti mjini Lisbon, Ureno, Novemba 12, 2025. (Xinhua)

Roboti ya Kampuni ya Roboti ya Unitree ikipeana ishara na washiriki kwenye Mkutano wa kilele wa Wavuti mjini Lisbon, Ureno, Novemba 12, 2025. (Xinhua)

LISBON – Banda la Maonyesho la Kampuni ya Roboti ya Unitree ya China kwenye Mkutano wa kilele wa Wavuti wa mwaka huu mjini Lisbon, Ureno limekuwa kama jukwaa dogo la maonyesho ya muziki, huku umati wa watu waliokuwa wamezunguka wakitazama roboti mahiri yenye umbo la binadamu ikishikana mikono na wageni, kuinama, kupiga ngumi hewani, na hatimaye kuanza kucheza ngoma chini ya taa zikitoa miale.

Rodriguez, mwanzilishi wa kampuni changa na bunifu kutoka Hispania, alisongea mbele kuipa mkono roboti hiyo, kupiga nayo picha, na kutikisa mwili kuendana na hatua zake za kucheza." Nilikuwa nimeona tu roboti za China mtandaoni. Hii ni mara yangu ya kwanza kuiona ana kwa ana -- ni ya kushangaza kabisa," amesema, huku akitikisa kichwa kwa kushangaa.

Kwa mujibu wa Wang Zhe, meneja wa kikanda wa kampuni ya Unitree, msambazaji bidhaa wa kampuni hiyo nchini Ureno ameshapokea maulizio mengi kwenye mkutano huo na tayari ameshauza makumi ya roboti nchini humo. "Kutakuwa na zaidi," ameongeza kwa kujiamini.

Roboti ya Kampuni ya Roboti ya Unitree ikipeana ishara na washiriki kwenye Mkutano wa kilele wa Wavuti mjini Lisbon, Ureno, Novemba 12, 2025. (Xinhua)

Roboti ya Kampuni ya Roboti ya Unitree ikipeana ishara na washiriki kwenye Mkutano wa kilele wa Wavuti mjini Lisbon, Ureno, Novemba 12, 2025. (Xinhua)

Msisimko huo unaotokana na roboti za Unitree unaonyesha ufuatiliaji unaozidi kuongezeka ambao uvumbuzi wa China unapokea kote duniani, vilevile ushirikiano wa kidijitali kati ya China na Ureno.

Mkutano wa mwaka huu pia unashirikisha kwa mara ya kwanza Mkutano wa kilele wa China, huku majukwaa na programu maalumu zikionyesha maendeleo ya China katika AI na mageuzi ya kiviwanda.

Miongoni mwa mambo yanayofuatiliwa katika mkutano huo ni uwepo wa ujumbe wa kampuni za teknolojia za China zikiwemo za Huawei, Alibaba, Tencent, na Unitree katika ushiriki wao wa pamoja kwa mara ya kwanza kwenye Mkutano huo.

"Kampuni hizi zinawakilisha uhai na uwezo wa biashara ya kidijitali na uchumi wa kidijitali wa China. Zimekuja kwa dhati, zikitafuta ushirikiano wa kunuifaishana na maendeleo ya pamoja," amesema Zhu Guangyao, afisa kutoka Wizara ya Biashara ya China.

Katika eneo la maonyesho la China, Huawei inaonyesha uwezo wake wa juu katika AI na huduma za wingu; Tencent inavutia umati wa watu kwa jukwaa lake la usanifu wa uchapishaji wa 3D; Alibaba inawasilisha huduma zake za kimataifa katika teknolojia ya wingu, AI, data kubwa, na huduma kwa makampuni.

Roboti yenye umbo la binadamu ikionyesha ustadi wake wa kukunja nguo kwenye Mkutano wa Intaneti Duniani (2025 WIC) Maonyesho ya Mwanga wa Intaneti mjini Wuzhen, Mkoani Zhejiang, mashariki mwa China, Novemba 6, 2025. (Xinhua/Huang Zongzhi)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha