China inayofungua mlango na inayojiendeleza, ni fursa na imani kwa dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 17, 2025

China inayofungua mlango na inayojiendeleza, ni fursa na imani kwa dunia

(I)

Maendeleo ya China hayawezi kutengana na Dunia, na ustawi wa dunia pia unahitaji kushirikiana na China. Ufunguaji mlango na ushirikiano wa kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja, ni ufunguo wa kuelewa maendeleo ya ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.

Maonyesho ya Nane ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) yalifungwa Novemba,10 mjini Shanghai. Maonyesho haya ya ngazi ya kitaifa ni ya kwanza duniani yenye mada ya uagizaji bidhaa, ambayo yalipangwa na Rais Xi Jinping mwenyewe. Maonyesho hayo ya mwaka huu yalifikia rekodi mpya, thamani ya jumla ya miamala imefikia dola za kimarekani bilioni 83.49 kwa mwaka, na kampuni 4,108 za kimataifa kutoka nchi na maeneo 138 zimeshiriki kwenye maonesho hayo.

Rais Xi alisema: "Mradi wa kujenga Bandari ya Biashara Huria ya Hainan kuwa eneo maalumu la usimamizi wa forodha utaanzishwa rasmi Desemba 18 mwaka huu, hii ni hatua muhimu ya alama ya China inayofungua mlango kithabiti na kuhimiza ujenzi wa uchumi ulio wa uwazi duniani.”

Kutoka hatua kubwa ya kujenga bandari ya biashara huria yenye umaalum wa China, hadi kuanzisha rasmi hatua ya alama ya kujenga kisiwa kizima cha Hainan kuwa eneo maalumu la usimamizi wa forodha, pamoja na lengo la kujenga eneo muhimu linaloongoza ufunguaji mlango wa China katika zama mpya”, ujenzi wa Bandari ya Biashara Huria ya Hainan umesonga mbele kwa hatua madhubuti katika mchakato wa mageuzi na ufunguaji mlango wa China.

Kujiendeleza kwa sambamba na kutafuta maendeleo kwa pamoja, dunia inashuhudia "mvuto wa China"kutokana na "nguvu hazijaonekana za China"katika soko kubwa, "msukumo wa China"na "utawala wa China"katika maendeleo ya sifa bora ya juu ya China.

(II)

"Nguvu hazijaonekana za China"zinahusu juhudi zetu za kuimarisha injini kuu ya matumizi, kuongeza uwezo wa ukuaji wa soko kubwa, na kufanya soko la China kuwa msingi wa kimkakati wa ujenzi wa mambo ya kisasa, na zaidi linaloweza kuleta fursa kubwa kwa dunia nzima na kutoa nafasi mpya kwa ajili ya maendeleo ya dunia.

"China imekuwa soko kubwa la pili la matumizi na uagizaji bidhaa duniani, ni nchi pekee inayoendelea ambayo inaandaa maonyesho ya kimataifa ya uagizaji bidhaa ya ngazi ya kitaifa, na kuendelea kufungua soko kwa dunia. "Rais Xi alisema.

China ina idadi ya watu zaidi ya bilioni 1.4, matumizi ya karibu yuan trilioni 50 ya kila mwaka, na kiasi cha uagizaji bidhaa unazidi yuan trilioni 20… kadiri kundi la watu wenye mapato ya kati linavyozidi kupanua na kundi la watumiaji vijana linavyojitokeza kwa kasi, utoaji bidhaa na mahitaji ya bidhaa zenye sifa bora zinaendana, ndivyo mahitaji ya jumla ya jamii yanavyoweza kuendelea kupanda ngazi ya juu, na mzunguko mkubwa wa mambo yote nchini unavyoongezwa msukumo zaidi.

Mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Uchumi Thomas Sargent alisema: "Uzoefu wa China umeonyesha kwamba, ufunguaji mlango ndio njia pekee ya kujenga utaratibu mpya wa jamii ulio wa utulivu na ulio wa kutarajiwa, ili watu wote wanaweza kupata manufaa. ”

(III)

"Msukumo wa China"unahusu chini ya uongozi wa uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, na uchumi halisi, kukuza nguvukazi mpya ya sifa bora kwa kufuata hali halisi ya kila sehemu, na kuharakisha ujenzi wa mfumo wa viwanda vya mambo ya kisasa.

Katika robo tatu za kwanza za mwaka huu, viwanda vya teknolojia ya juu nchini China kihalisi vilitumia mitaji ya kigeni ya yuan bilioni 170.84. Hivi sasa uvumbizi unaonekana hali yake mpya katika sekta nyingi nchini China, gharama za uvumbuzi zimepungua zaidi, na kupata faida kubwa zaidi, ambapo idadi kubwa zaidi duniani ya timu za utafiti na maendeleo, makundi mengi zaidi yaliyoko kwenye safu ya makundi ya 100 bora ya uvumbuzi pamoja na kiwango cha uvumbuzi kinachochukua nafasi ya 10 duniani.

Kutoka "kiwanda cha dunia"hadi "chimbuko la uwezo mpya wa uvumbuzi na matunda ya uvumbuzi”, kutoka "kufanya biashara kote duniani"hadi "kuchangia maendeleo ya dunia"China imekuwa soko la kimkakati la uvumbuzi wa dunia na injini muhimu ya ukuaji.

(IV)

"Mvuto wa China"unahusu China inayodumisha utulivu wa hali ya siasa kwa muda mrefu, na utulivu wa jamii, kujenga mazingira ya sera yalio wazi, ya utulivu, na yanayoweza kutarajiwa, na kufanya juhudi za kujenga mazingira ya biashara ya kiwango cha juu, kufanya "Utawala wa China"kuwa nguvu laini muhimu ya China.

Rais Xi alifafanua, "China inaendelea kujenga mazingira ya biashara ya kiwango cha juu ya soko huria, kwa mujibu wa sheria na hali ya kimataifa, kuhimiza ushindani wa usawa kati ya kampuni za umilikaji wa aina mbalimbali ili kupata maendeleo kwa pamoja.""China inajulikana kuwa moja ya nchi zenye usalama zaidi duniani, na imetoa sera za msamaha wa visa wa upande mmoja au kusameheana kwa pande zote kwa nchi 76. "Hii pia ni sababu muhimu ya mvuto wa China inayofungua mlango na inayojiendeleza.

"Zamani ufunguaji mlango wetu ulikuwa wa ‘kufuata nchi nyingine’, sasa unakuwa wa ‘kuongoza nchi nyingine’, huu ndio ufunguaji mlango wa kiwango cha juu zaidi."China inayoshikilia kuhimiza ufunguaji mlango kwenye kiwango cha juu, hakika italeta hali ya uhakika na nguvu zaidi kwa dunia nzima.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha