Lugha Nyingine
Mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Marburg waripotiwa kusini mwa Ethiopia
Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika (Africa CDC) kimetambua uthibitishaji wa Wizara ya Afya ya Ethiopia na Taasisi ya Afya ya Umma ya Ethiopia (EPHI) juu ya mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Marburg katika eneo la Jinka kusini mwa nchi hiyo.
Taarifa iliyotolewa na Africa CDC siku ya Jumamosi imesema, uchunguzi zaidi wa magonjwa ya mlipuko na uchambuzi wa kimaabara wa data bado unaendelea, na aina ya virusi hivyo iliyogunduliwa inaonesha mfanano na vile vilivyogunduliwa awali katika nchi za Afrika Mashariki.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Wizara ya Afya ya Ethiopia, Taasisi ya Afya ya Umma ya Ethiopia na idara za afya za kikanda zimeanzisha hatua za kukabiliana na mlipuko huo, ikiwa ni pamoja na kuongeza ufuatiliaji, uchunguzi wa kwenye maeneo husika, kuimarisha juhudi za kuzuia na kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo na juhudi za kushirikisha jamii.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



