Lugha Nyingine
Serikali ya DRC na waasi wa M23 wasaini makubaliano ya mfumokazi kuelekea makubaliano ya amani
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kundi la waasi wa M23 wamesaini makubaliano ya mfumokazi, ikiashiria hatua mpya kuelekea makubaliano ya amani yanayolenga kumaliza mapigano mashariki mwa DRC.
Katika taarifa iliyotolewa Jumamosi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imesema makubaliano hayo yamefikiwa kutokana na msukumo wa Azimio la Kanuni lililosainiwa na pande hizo mbili Julai 19 ambalo lilisisitiza tena dhamira zao za kushughulikia chanzo cha mapigano kupitia majadiliano yaliyopangiliwa, hatua za kujenga kuaminiana, na mbinu ya kupunguza mvutano na kuleta utulivu kwa awamu.
Wizara hiyo imesema, makubaliano hayo ya mfumokazi yatatumika kama nyaraka rejea ya kimsingi kwa mchakato mpana wa amani.

Mpatanishi mkuu wa Qatar Mohammed al-Khulaifi (kulia) akitazama huku Sumbu Sita Mambu (katikati), mwakilishi wa ngazi ya juu wa mkuu wa nchi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) akisaini nyaraka katika hafla ya kusaini Makubaliano ya Kina ya Amani kati ya Serikali ya DRC na Muungano wa Mto Kongo/Vuguvugu la Machi 23 (AFC/M23) kwenye Hoteli ya Sheraton mjini Doha, Novemba 15, 2025. (Picha na Mahmud HAMS/cfp)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



