Lugha Nyingine
Reli ya mwendokasi inayounganisha kituo cha zamani cha mapinduzi ya China na Mji wa Xi'an yaanza kufanya kazi kwa majaribio (3)
XI'AN - Reli ya mwendokasi inayounganisha Xi'an, mji mkuu wa Mkoa wa Shaanxi, kaskazini magharibi mwa China, na Mji wa Yan'an upande wa kaskazini mwa Shaanxi imeingia katika kipindi chake cha uendeshaji wa majaribio, ikimaanisha kupiga hatua muhimu kuelekea uendeshaji wake wa kawaida.
Kipindi hicho cha uendeshaji wa majaribio kimeanza jana Jumatatu asubuhi wakati treni ya uendeshaji wa majaribio No. 55302 ilipoondoka Xi'an kuelekea Yan'an -- ikibadilika kutoka kipindi cha uendeshaji wa kubaini matatizo na upimaji kwa pamoja hadi kipindi cha kuigilizia uendeshaji wa kawaida.
Reli hii ni reli ya kwanza ya mwendokasi katika kituo cha zamani cha mapinduzi ya China cha kaskazini mwa Shaanxi, urefu wake umefikia kilomita 299.8 na kasi yake ilisanifiwa kuwa ya kilomita 350 kwa saa na imepunguza muda wa safari kati ya Xi'an na Yan'an kutoka saa 2.5 hadi saa moja hivi.
Yan'an ni mji wenye umuhimu mkubwa wa kihistoria -- kwani ulikuwa kituo cha uongozi wa mapinduzi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kuanzia mwaka 1937 hadi mwaka 1947.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




