Mkoa wa Shandong wa China waendeleza nishati za kijani ili kusukuma mbele kubadilisha muundo mpya wa nishati (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 21, 2025
Mkoa wa Shandong wa China waendeleza nishati za kijani ili kusukuma mbele kubadilisha muundo mpya wa nishati
Wafanyakazi wakipaka rangi sehemu za katikati za jenereta ya kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo kwenye karakana ya kupaka rangi ya eneo maalum la viwanda vya kutengeneza zana na vifaa vya kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo katika Wilaya ya Huimin, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China, Novemba 19, 2025. (Xinhua/Guo Xulei)

Mwaka 2020, China ilitangaza kwamba itajitahidi kufikia kilele cha kutoa hewa ya kaboni dioksidi kabla ya mwaka 2030 na msawazisho wa kaboni kabla ya mwaka 2060.

Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China katika miaka ya hivi karibuni umekuwa ukifanya juhudi kubwa ili kufikia malengo hayo mawili. Mkoa huo wa pwani unatumia nguvu yake bora ya hali ya topografia kwa kuendeleza nishati za kijani kwenye maeneo yake ya nchi kavu na baharini, na wakati huohuo ukijenga miundombinu ya nishati isiyo ya visukuku.

Mkoa huo unapanga mradi unaofungamanisha uhifadhi na usambazaji wa nishati za upepo na jua kwenye eneo la mawimbi lenye chumvi na alkali, na kituo cha nishati safi kinachotegemea zaidi umeme unaotokana na nishati ya jua katika maeneo ya migodi ya makaa ya mawe yenye hali ya kuhama kwa matabaka ya miamba chini ya ardhi.

Wakati huo huo, mkoa huo wa Shandong umefanya juhudi kubwa za kujenga viwanda vya zana na vifaa vya nishati, ukianzisha mazingira mazuri kwa maendeleo ya hali ya kubadilisha muundo mpya wa nishati na maendeleo ya viwanda vya zana na vifaa vya nishati.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha