Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Kabila la Waqiang yasherehekewa katika Mkoa wa Sichuan, Kusini-Magharibi mwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 21, 2025
Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Kabila la Waqiang yasherehekewa katika Mkoa wa Sichuan, Kusini-Magharibi mwa China
Maonyesho ya Opera ya Sichuan yakifanyika katika shughuli za kusherehekea Mwaka Mpya wa Kabila la Waqiang katika Wilaya ya Wenchuan, Eneo linalojiendesha la Makabila ya Watibeti na Waqiang la Aba, Mkoa wa Sichuan, kusini-magharibi mwa China, Novemba 19, 2025. (Picha na Lan Hongguang/Xinhua)

Shughuli ya kusherehekea Mwaka Mpya wa Kabila la Waqiang imefanyika katika Wilaya ya Wenchuan, Mkoa wa Sichuan, kusini-magharibi mwa China Jumatano, ikiwa mwanzo wa kuanzishwa kwa shughuli mbalimbali za kusherehekea Mwaka Mpya wa huo wa jadi wa kabila la Waqiang, ambao uliwadia jana Novemba 20 kwa mwaka huu.

Watu wa Kabila la Waqiang, moja ya makabila ya kale zaidi ya China, mara nyingi huchukuliwa kuwa ni "kisukuku hai" katika historia ya maendeleo ya Taifa la China. Mkoa huo wa Sichuan ni sehemu pekee nchini China wanakokusanyika na kuishi watu wa kabila la Waqiang.

Kila mwaka, katika siku ya kwanza ya mwezi wa 10 kwa kalenda ya kilimo ya China, watu wa kabila la Waqiang wanasherehekea sikukuu yao hiyo muhimu zaidi ya jadi -- Mwaka Mpya wa Kabila la Waqiang. Wakati wa sikukuu hiyo, Waqiang wanafanya shughuli mbalimbali za mada ya kuabudu mbingu na kutoa shukrani, wakifanya hafla mbalimbali za matambiko ya kuheshimu miungu, kufukuza mambo mabaya na yenye kuleta mikosi, kutoa shukrani kwa mavuno, na kuombea heri na baraka.

Sikukuu hiyo ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kabila la Waqiang iliongezwa na UNESCO kwenye Orodha yake Wakilishi ya Mali ya Urithi wa Utamaduni Usioshikika wa Binadamu mwaka 2024.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha