Lugha Nyingine
Ndoto za Ujasiriamali za Vipaji vya Kimataifa zaanzia kwenye Kituo cha Nyumba ya Vipaji mkoani Hainan, China (7)
"Mwanzoni kabisa, kama raia wa kigeni, sikujua chochote, na alinipeleka sehemu nyingi kwa ajili ya kutembelea na kujifunza, na kunisaidia kujenga mtandao na washirika, msaada niliopokea kwenye kituo hiki umenisaidia sana.” Amesemea Amissah Richard Frank, mjasiliamali kutoka Ghana anayeishi Haikou, Mji Mkuu wa Mkoa wa Hainan wa China. Mtu huyo, aliyekuwa akimrejelea kumsaidia, ni meneja wa Kituo cha Nyumba ya Vipaji vya Kimataifa ya Haikou, Pi Jinyu. Chini ya msaada wa kituo hicho, kampuni ya biashara ya Frank ilikua kwa kasi ndani ya mwaka mmoja tu, na anauchukulia Mji wa Haikou kuwa “ni sehemu kama nyumbani” kwake.
Ujenzi wa Bandari ya Biashara Huria ya Hainan uko katika hali motomoto, ikivutia vipaji vingi vya kimataifa kwenda huko na kukimbiza ndoto zao. Katika miaka ya hivi karibuni, Mji huo wa Haikou umetoa kipaumbele kwa kazi ya kuingiza, kuhudumia na kusimamia vipaji, ikiboresha kila wakati urahisi wa kazi na maisha yao na kujenga kwa bidii ‘makazi’ kwa vipaji vya kimataifa kukimbiza ndoto.
Mwaka 2021, chini ya mwongozo wa Idara ya Teknolojia na Maendeleo ya Habari za Viwanda ya Haikou, jukwaa la huduma kwa vipaji vya kimataifa la “Nyumba ya Vipaji vya Kimataifa ya Haikou”, lilianzishwa. Wageni wengi wanaoishi Haikou wameanzisha ndoto zao za ujasiriamali kutokea kwenye kituo hicho.
Hadi Oktoba 2025, kituo hicho kwa jumla kilikuwa kimevutia vipaji vya kimataifa zaidi ya 500 katika Mji wa Haikou, kufanya kwa mafanikio madarasa matano ya mafunzo ya kukuza ujasiliamali kwa vipaji vya kimataifa, kutoa huduma au kukuza vipaji kwa mara zaidi ya 200, na kuvisaidia kwa mafanikio vipaji vya kimataifa kuanzisha kampuni karibu 50.
Vilevile, vipaji hivi vya kigeni pia vinakumbatia mji huo kwa njia yao wenyewe. Mwaka 2023, profesa mstaafu wa Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Singapore Foo Check Woo na mkewe walivutiwa na mustakabali unaozidi kuongezeka wa ustawi wa bandari ya biashara huria ya Hainan, na kuamua kuhamia Haikou, wakitumai kusaidia wageni wengi zaidi kuzoea maisha huko kwa kupitia huduma za kujitolea. “Nyumbani kwa mababu zangu ni Mji wa Wenchang, Hainan, na ni heshima kufanya jambo kwa vijana wa nyumbani kwangu,” amesema Foo.
Agosti, 2024, Timu ya Huduma za Kujitolea ya Vipaji vya Kimataifa ya Haikou ilianzishwa rasmi, ikiendeshwa na Nyumba ya Vipaji vya Kimataifa ya Haikou. Kwa sasa timu hiyo imevutia washiriki 65 wa kimataifa akiwemo Foo.
Pi amesema, baada ya Bandari ya Biashara Huria ya Hainan kuwa eneo maalumu la usimamizi wa forodha mwezi Desemba mwaka huu, raia zaidi wa kigeni kutoka sehemu mbalimbali duniani watafuatilia Hainan na kwenda Hainan. “Tupo tayari kuwapa huduma nyingi zaidi, bora zaidi na zenye ukarimu zaidi, ili kuwasaidia kufikia ndoto zao mkoani Hainan.”
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




