Rais wa Guinea-Bissau aishukuru China kwa msaada wa zana na vifaa vya usalama wa uwanja wa ndege

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 24, 2025
Rais wa Guinea-Bissau aishukuru China kwa msaada wa zana na vifaa vya usalama wa uwanja wa ndege
Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalo (kushoto, mbele) na Balozi wa China nchini Guinea-Bissau Yang Renhuo (kulia, mbele) kwa pamoja wakikagua zana na vifaa vya ukaguzi wa usalama wa uwanja wa ndege vilivyotolewa na China mjini Bissau, Novemba 21, 2025. (Xinhua/Si Yuan)

BISSAU - Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalo ametoa shukrani kwa msaada muhimu wa China wakati akishiriki kwenye hafla ya kukabidhiwa zana na vifaa vya ukaguzi wa usalama wa Uwanja wa Ndege vilivyotolewa na China katika mji mkuu Bissau siku ya Ijumaa.

Waziri Mkuu wa Guinea-Bissau, Braima Camara, Waziri wa Mawasiliano Marciano Silva Barbeiro na maofisa wengine waandamizi wa Bissau-Guinea, pamoja na wajumbe wa nchi zote mbili, walishiriki kwenye hafla hiyo.

Embalo na Balozi wa China nchini Guinea-Bissau Yang Renhuo walizindua zana kwa pamoja, baada ya hapo Yang na Barbeiro walisaini cheti cha kukabidhiwa kwa zana na vifaa.

Katika hotuba yake, Rais Embalo amesema msaada huo si tu utainua dhahiri kiwango cha mambo ya kisasa ya huduma katika uwanja huo wa ndege wa Guinea-Bissau bali pia umeonesha wazi urafiki mkubwa kati ya nchi hizo mbili.

Ameongeza kuwa zana na vifaa hivyo vitabeba jukumu muhimu katika kuimarisha usalama wa usafiri ndege wa nchi hiyo.

Ubalozi wa China nchini Guinea-Bissau umejulisha kuwa, seti hiyo ya zana za mfumo wa ukaguzi wa usalama unahusisha kazi mbalimbali za uchunguzi wa usalama, upigaji picha kwa teknolojia ya kisasa, kufanya uchambuzi kwa teknolojia ya AI na data kubwa. Zana hizo zikilinganishwa na nyingine za jadi, mfumo wake mpya unaweza kuwa na ufanisi wa juu zaidi na kujikagua na kugundua kwa usahihi zaidi vitu hatari na vilivyopigwa marufuku.

Ubalozi wa China nchini humo umeongeza kuwa mara tu zana na vifaa hivyo vitakapoanza kufanya kazi, vinatarajiwa kusaidia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Osvaldo Vieira kuinua kiwango chake cha usimamizi wa kutumia teknolojia za kidijitali na za kisasa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha