Ni ukweli usiopingika kwamba kuna China moja tu, na Taiwan ni sehemu yake: Wizara ya Mambo ya Nje ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 26, 2025

BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning amesema kwamba ni ukweli usiopingika ambao hauwezi kupotoshwa au kubadilishwa kwamba kuna China moja tu duniani, na Taiwan ni sehemu isiyoweza kutenganishwa ya nchi ya China.

Msemaji Mao alisema hayo jana Jumanne alipojibu maoni ya watu wachache nchini Japan waliosema kwamba ni Jamhuri ya China, si Jamhuri ya Watu wa China, iliyokubali Japan kujisalimisha, kwa hivyo maoni ya watu hao ni kwamba Jamhuri ya Watu wa China haina haki ya kujadili suala la Taiwan.

"Wale wanaotoa maoni kama hayo ama hawajui historia au kwa makusudi wanatafuta kuipotosha na kupuuza sheria za kimataifa," msemaji Mao ameuambia mkutano na waandishi wa habari.

Msemaji huyo amesema, "Mwaka 1945, Japan ilisaini Nyaraka ya Kujisalimisha, ambayo kwayo iliahidi kwamba itatimiza kwa uaminifu wajibu uliowekwa kwenye Tangazo la Potsdam na kuirudisha Taiwan kwa China bila masharti," na China ilikabidhiwa tena mamlaka yake juu ya Taiwan na kurudisha Taiwan kisheria na kivitendo.

Amesema mwaka 1949, serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ilichukua nafasi ya serikali ya Jamhuri ya China.

Haya ni mabadiliko ya serikali ambayo kwayo China, ikiwa nchi mhusika mkuu wa sheria ya kimataifa haikubadilika, na mamlaka ya nchi na mipaka ya aridhi ya kudumu ya China haijabadilika ," amesema.

Msemaji amesema, "Ndio maana, hakika serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ina haki kikamilifu ya kutekeleza mamlaka ya nchi ya China, ikiwa ni pamoja na mamlaka juu ya eneo la Taiwan."

Mao ameongeza kuwa Taarifa ya Pamoja kati ya China na Japan ya mwaka 1972 inasema kwamba Serikali ya Japan inatambua Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ni Serikali pekee halali ya China.

"Kuna China moja tu duniani. Taiwan ni sehemu isiyoweza kutenganishwa ya nchi ya China. Huu ni ukweli usiopingika ambao hauwezi kupotoshwa au kubadilishwa," msemaji huyo amesema.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha