Lugha Nyingine
Sekta ya viwanda yastawi katika Mji wa Wuhu, Mashariki mwa China

Fundi akirekebisha roboti ya kisasa ya viwandani kwenye Kampuni ya Roboti za AI ya Efort mjini Wuhu, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China, Novemba 21, 2025. (Xinhua/Liu Junxi)
Mji wa Wuhu katika Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China ni kituo muhimu cha viwanda vya utengenezaji wa bidhaa, viwanda hivyo vinahusisha aina 37 kati ya aina 41 za viwanda vya China. Viwanda vyake muhimu ni pamoja na vya kuunda magari, nishati ya kijani, na vyombo vya umeme vya matumizi ya nyumbani, ambavyo kila kiwanda hutoa thamani ya uzalishaji wa mwaka inayofikia yuan bilioni 100 (dola za Marekani karibu bilioni 14).
Mji huo pia umeshuhudia kuongezeka kwa haraka kwa viwanda vya roboti katika miaka ya hivi karibuni kutokana na maendeleo ya teknolojia za AI na msingi imara wa viwanda wa mji huo.
Kundi la viwanda vya roboti vya ngazi ya kitaifa linaanza kuonekana katika mji huo, huku kampuni za viwanda zaidi ya 300 zikichangia mnyororo jumuishi wa viwanda wenye thamani ya yuan bilioni 40 (Dola za Marekani karibu dola milioni 563) mwaka 2024.

Picha iliyopigwa Novemba 21, 2025 ikionyesha mfanyakazi akifanya kazi kwenye karakana ya Kampuni ya Roboti za AI ya Efort mjini Wuhu, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China. (Picha na Zhao Xianfu/Xinhua)

Fundi akirekebisha roboti ya teknolojia ya kisasa ya viwandani kwenye Kampuni ya Roboti za AI ya Efort mjini Wuhu, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China, Novemba 21, 2025. (Xinhua/Liu Junxi)

Picha iliyopigwa Novemba 21, 2025 ikionyesha fundi akirekebisha roboti ya viwandani kwenye karakana ya kufanya majaribio ya Kampuni ya Roboti za AI ya Efort mjini Wuhu, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China (Picha na Zheng Xianlie/Xinhua)

Roboti ya kupima ubora inayotumia teknolojia ya AI ikifanya kazi kwenye kiwanda cha teknolojia za kisasa cha Kampuni ya Kuunda Magari ya Chery ya China mjini Wuhu, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China, Septemba 12, 2024. (Xinhua/Zhang Rui)

Roboti ya viwandani ikifanya kazi kwenye mstari wa uzalishaji wa teknolojia za kisasa wa Kampuni ya Teknolojia ya Zenner Metering katika eneo la maendeleo ya uchumi la Xinwu mjini Wuhu, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China, Novemba 13, 2025. (Picha na Xiao Benxiang/Xinhua)

Roboti ya viwandani ikifanya kazi kwenye mstari wa uzalishaji wa teknolojia za kisasa wa kiwanda cha Kampuni ya Kuunda Magari ya Chery ya China mjini Wuhu, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China, Septemba 12, 2024. (Xinhua/Liu Junxi)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



