Lugha Nyingine
Shule ya mfano wa elimu ya afya kuhusu kichocho yafunguliwa nchini Tanzania
Timu ya wataalamu ya kuzuia na kudhibiti kichocho inayofadhiliwa na China visiwani Zanzibar, Tanzania hivi karibuni imeipa Shule ya Msingi ya Matungu katika Kisiwa cha Pemba hadhi ya kuwa shule ya mfano wa elimu ya afya ya kupambana na kichocho katika hafla iliyofanyika katika Kisiwa cha Pemba.
Washiriki zaidi ya 200 walihudhuria hafla hiyo, wakiwemo viongozi wa serikali na afya wa Kisiwa cha Pemba, viongozi kutoka Mkoa wa Jiangsu wa China, wawakilishi kutoka sekta ya elimu ya Pemba, pamoja na walimu na wanafunzi.
Mkurugenzi Msaidizi wa Kamati ya Afya ya Mkoa wa Jiangsu Zhou Minghao, ameipongeza Shule ya Msingi ya Matungu kwa mafanikio yake makubwa yaliyopatikana wakati wa kipindi cha miaka miwili iliyopita katika kuhimiza elimu ya afya ya kupambana na kichocho.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Bw. Rashid Hadidi Rashid ameishukuru China kwa msaada wake wa muda mrefu, akisema kuwa kichocho ni changamoto kubwa kwa afya ya umma katika mkoa wake.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



