Mawaziri wa nchi za Afrika Mashariki wakubali kuimarisha ulinzi wa wakimbizi

(CRI Online) Novemba 28, 2025

Mawaziri kutoka Mamlaka ya Kiserikali juu ya Maendeleo ya Nchi za Afrika Mashariki (IGAD), jana Alhamisi wamepitisha taarifa ya kuimarisha ulinzi na ujumuishwaji wa kiuchumi na kijamii kwa wakimbizi.

Mawaziri hao, waliokutana kwenye mkutano mjini Nairobi, wamesisitiza kuwaunga mkono waathirika wa vita na wale waliokimbia makazi yao kutokana na mabadiliko ya tabianchi kwa kupitia kuratibu sera na sheria huku wakichangia mifano ya mafanikio ya kuwajumuisha upya watu hao katika jamii.

Waziri wa Mambo ya Ndani na Uratibu wa Taifa wa Kenya, Onesmus Murkomen, amesema eneo la IGAD linakabiliana na msukosuko wa wakimbizi unaohitaji juhudi za pamoja, na kwamba eneo la Pembe ya Afrika kwa sasa limekuwa na wakimbizi karibu milioni sita, ambao wameleta shinikizo kubwa kwa mifumo ya ikolojia na uchumi wa nchi zinazowapokea.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha