Kenya yadhamiria kuongeza ushirikiano na China ili kuboresha miundombinu

(CRI Online) Novemba 28, 2025

(Picha/VCG)

(Picha/VCG)

Rais William Ruto wa Kenya amesema serikali yake itaendelea kuongeza ushirikiano na China kwa moyo wa ushirikiano na maendeleo ya pamoja.

Akiukaribisha ujumbe kutoka Benki ya Exim ya China ulioongozwa na mwenyekiti wake Bw. Chen Huaiyu mjini Nairobi jana Alhamisi, Rais Ruto amesema uwepo unaoongezeka wa mashirika ya China nchini Kenya unaonyesha imani yao kwa utulivu wa nchi na utayari wao wa kupanua uwekezaji.

Pia amesema Benki ya Exim ya China ni nguzo muhimu ya ushirikiano, na Kenya inathamini uungaji wake mkono endelevu kwa miradi mikubwa ya miundombinu, pamoja na ukuaji wa programu za elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.

Bw. Chen amesisitiza kuwa benki hiyo ina dhamira thabiti ya kuendeleza ushirikiano na Kenya, akibainisha kwamba China inaendelea kuwa na nia ya kuhimiza uhusiano wa kiuchumi na kibiashara na kunufaisha Wakenya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha