Lugha Nyingine
Kuhusu ujasiliamali kisiwani Hainan, vipaji vya kimataifa vimesema...
Tarehe 17, Novemba, katika Kituo cha Nyumba ya Vipaji vya Kimataifa ya Haikou, vipaji kadhaa vya kimataifa vilichangia maoni na hisia zao kuhusu huduma na sera za vipaji za Hainan na waandishi habari wa People’s Daily Online.
Mwaka 2021, chini ya mwongozo wa Idara ya Teknolojia na Maendeleo ya Habari za Viwanda ya Haikou, jukwaa la huduma kwa vipaji vya kimataifa la "Nyumba ya Vipaji vya Kimataifa ya Haikou", lilianzishwa. Wageni wengi wanaoishi Haikou wameanzisha ndoto zao za ujasiriamali kutokea kwenye kituo hicho.
Hadi Oktoba 2025, kituo hicho kwa jumla kilikuwa kimevutia vipaji vya kimataifa zaidi ya 500 katika Mji wa Haikou, kufanya kwa mafanikio madarasa matano ya mafunzo ya kukuza ujasiliamali kwa vipaji vya kimataifa, kutoa huduma au kukuza vipaji kwa mara zaidi ya 200, na kuvisaidia kwa mafanikio vipaji vya kimataifa kuanzisha kampuni karibu 50.

Darasa la kipindi cha tano la ujasiliamali kwa vipaji vya kimataifa likifanywa na Kituo cha Nyumba ya Vipaji vya Kimataifa ya Haikou, Juni, 2025. (Picha na Kituo cha Nyumba ya Vipaji vya Kimataifa ya Haikou)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



