Lugha Nyingine
PMI ya viwanda ya China yaongezeka, ikiashiria kuimarika kwa imani ya soko

Mhandisi akitazama roboti yenye umbo la binadamu ikichukua kifaa kwenye maabara ya Kampuni ya Mambo ya Roboti ya Leju mjini Hefei, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China, Oktoba 24, 2025. (Xinhua/Zhou Mu)
BEIJING – Kielezo cha mameneja wa ununuzi (PMI) kwa sekta ya viwanda ya China kilikuwa 49.2 mwezi Novemba, ongezeko la asilimia 0.2 kutoka mwezi uliopita, takwimu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) zimeonyesha jana Jumapili. Kielezo hicho kikiwa juu ya 50 unaonyesha upanuzi, na kikiwa chini ya 50 unaonyesha kusinyaa kwa sekta hiyo.
NBS imesema pande zote mbili za uzalishaji na mahitaji zilishuhudia maboresho huku kielezo kidogo cha uzalishaji kikiwa 50.0, ongezeko la asilimia 0.3 kutoka mwezi uliopita -- ikifikia kikomo muhimu. Kwa upande wa mahitaji, kielezo kidogo cha oda mpya kilikuwa 49.2, ongezeko la asilimia 0.4.
Kuhusu viwanda maalum, takwimu hizo zinaonyesha kwamba vielezo vya uzalishaji na oda mpya kwa sekta kama vile usindikaji wa chakula cha kilimo na uchenjuaji wa metali isiyo na madini ya chuma vilikuwa katika eneo la upanuzi, ikionyesha uzalishaji na mahitaji katika hali nzuri.
Takwimu hizo pia zinaonyesha kwamba PMI kwa kampuni ndogo ilishuhudia ongezeko kubwa, ikiwa katika 49.1 – ongezeko la asilimia 2 kutoka mwezi uliopita hadi kufikia kiwango cha juu katika miezi sita, wakati huohuo PMI kwa kampuni kubwa ilikuwa katika 49.3, ambayo ni kushuka kwa asilimia 0.6, huku kielezo hicho cha kampuni za ukubwa wa kati kikiwa katika 48.9, ongezeko la asilimia 0.2.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, matarajio ya soko yaliendelea kuwa tulivu na mwelekeo wa kupanda kidogo. Kielezo kidogo cha matarajio ya shughuli za uzalishaji na uendeshaji kilikuwa katika 53.1, ongezeko la asilimia 0.3 kutoka Oktoba, ikionyesha kwamba kampuni za kiviwnada zimekua na imani zaidi katika maendeleo ya hivi karibuni ya soko.
Zhang Liqun, mchambuzi katika Shirikisho la Usafirishaji na Ununuzi la China (CFLP), amebainisha kuwa kuimarika huko kidogo kwa PMI ya Novemba kunaonyesha kuboreka kwa imani ya soko.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



