Kipindi cha muziki cha“Sing for Africa” kinachodhaminiwa na China chaangazia waimbaji wanaochipukia wa Kenya

(CRI Online) Desemba 01, 2025

Wasanii wanaochipukia zaidi ya 500 wameshiriki kwenye majaribio ya awali ya kuchagua vipaji vya muziki kwa ajili ya kipindi cha “Sing for Africa” kinachodhaminiwa na China jana Jumapili katika Chuo Kikuu cha Nairobi, Kenya.

Kipindi hicho cha muziki kilizinduliwa tarehe 12 Novemba mwaka huu kwa ushirikiano kati ya Chaneli ya Kimataifa ya Televisheni ya Hunan ya China na mshirika wake chombo cha habari cha nchini humo. Washiriki walionyesha ujuzi wao katika aina mbalimbali za muziki.

Kipindi hicho kinacholenga kukuza waimbaji wanaochipukia na kuimarisha ushirikiano wa kiutamaduni kati ya China na Afrika, kinahusisha majaribio ya awali ya wazi ya kuchagua washiriki, raundi za mtoano na fainali kuu. Licha ya tuzo ya fedha, mshindi atalipiwa ziara ya kumuziki nchini China, na kusaini makubaliano ya kurekodi nyimbo na watayarishaji mashuhuri.

"Onesho hili si tu ni daraja kati ya wakenya, bali pia kati ya watu wa Afrika na China. Litafungua milango kwa wasanii kupitia programu za mabadilishano kati ya Afrika na China" mshiriki Jave Samson Mwavita amesema.

Ameongeza kuwa, onyesho hilo litasaidia wasanii wenyeji wajionee utamaduni wa China, kuhimiza mafungamano ya kitamaduni, kuwaunganisha na studio zinazoongoza za kurekodi, na kuwapeleka kwenye viwango vipya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha