Mkutano wa Uwekezaji wa Madini wa Afrika Mwaka 2026 wafanyika nchini Afrika Kusini

(CRI Online) Februari 11, 2026

Watu wakitembelea eneo la maonyesho ya madini la Mkutano wa Uwekezaji wa Madini wa Afrika 2026, mjini Cape Town, Afrika Kusini, Februari 9.

Watu wakitembelea eneo la maonyesho ya madini la Mkutano wa Uwekezaji wa Madini wa Afrika 2026, mjini Cape Town, Afrika Kusini, Februari 9. (Picha/Xinhua)

Mkutano wa siku nne wa Uwekezaji wa Madini wa Afrika Mwaka 2026 umefunguliwa mjini Cape Town, Afrika Kusini, ambapo utajumuisha mazungumzo kadhaa ya ngazi ya juu kati ya serikali za nchi, mikutano ya uwekezaji, mijadala na semina.

Akihutubia hafla ya ufunguzi wa mkutano huo, Waziri wa Madini na Rasilimali za Mafuta wa nchi hiyo, Gwede Mantashe amesema, mvutano wa siasa za kijiografia umekuwa ukiongezeka kutokana na baadhi ya makundi ya kiuchumi yaliyoendelea kujaribu kudhibiti rasilimali za asili za nchi zinazoendelea.

Ametoa wito kwa nchi zote kuhimiza ushirikiano, na kuharakisha mchakato wa utafutaji na uchimbaji madini kwa uwajibikaji, ili kuhakikisha Afrika inaweza kupata thamani kubwa zaidi kutokana na rasilimali zake za madini.

Picha hii iliyopigwa Februari 9 ikionyesha eneo la maonyesho ya madini la Mkutano wa Uwekezaji wa Madini wa Afrika 2026, mjini Cape Town, Afrika Kusini.

Picha hii iliyopigwa Februari 9 ikionyesha eneo la maonyesho ya madini la Mkutano wa Uwekezaji wa Madini wa Afrika 2026, mjini Cape Town, Afrika Kusini. (Picha/Xinhua)

Waziri wa Madini na Rasilimali za Mafuta wa Afrika Kusini, Gewede Mantashe, akitoa hotuba kwenye hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Uwekezaji wa Madini wa Afrika 2026 mjini Cape Town, Afrika Kusini, Februari 9.

Waziri wa Madini na Rasilimali za Mafuta wa Afrika Kusini, Gewede Mantashe, akitoa hotuba kwenye hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Uwekezaji wa Madini wa Afrika 2026 mjini Cape Town, Afrika Kusini, Februari 9. (Picha/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha