China yapinga Marekani kutunga visingizio ili kutaka kuanza kwake tena majaribio ya silaha za nyuklia

(CRI Online) Februari 12, 2026

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China Lin Jian amesema shutuma za Marekani kwa majaribioya nyuklia ya China, ni zisizo na msingi kabisa na kwamba China inapinga Marekani kutunga sababu ili kutaka kuanza kwake tena majaribio ya silaha za nyuklia.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari mapema wiki hii, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Dina Powell alitoa wito kwa China kushiriki kwenye mazungumzo ya pande nyingi ya kudhibiti silaha za nyuklia na utulivu wa kimkakati.

Akizungumzia suala hilo jana Jumatano msemaji huyo amesisitiza kuwa, China siku zote inafuata njia ya maendeleo ya amani, na inatekeleza sera ya nyuklia ya kujilinda yenye lengo la kudumisha utulivu wa muda mrefu. Pia amesisitiza kuwa China itaendelea kuchangia katika kulinda amani na usalama duniani.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha