Lugha Nyingine
Mashindano ya Wushu ya China na Afrika yafunguliwa nchini Misri
Mashindao ya 7 ya Wushu Kung Fu ya Vijana ya Afrika yamefunguliwa Jumanne wiki hii katika mji mkuu wa Misri, Cairo, na kukutanisha wanamichezo, makocha, na maofisa karibu 100 kutoka nchi mbalimbali za Afrika pamoja Timu ya Taifa ya Wushu ya China.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa mashindano hayo, Rais wa Shirikisho ya Wushu Kung Fu la Afrika, Sherif Mostafa amesema, mchezo huo unazingatia amani na nidhamu binafsi na kwamba mashindano hayo yanatumika kama jukwaa la maendeleo ya vijana na pia kama daraja kati ya urithi wa Afrika na sanaa ya Kung Fu ya China.
Naye Konsuli wa Ubalozi wa China nchini Misri, Zhang Yaqiang ameielezea Wushu kuwa ni hazina kubwa ya utamaduni wa China, na kusisitiza umuhimu wa mabadilishano ya kati ya watu na watu.
“Vyote Sanaa ya Wushu ya China na michezo ya jadi ya Afrika vinaakisi thamani ya pamoja ya kustahimili mambo magumu na ujasiri katika kukabiliana na changamoto,” amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



