Hali ya Mchipuko kwenye barafu na theluji: “Uchumi wa Hali Moto Moto” kwenye ardhi nyeusi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 12, 2026

Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na ukuaji wa mambo ya utamaduni na viwanda yanayohusika na barafu na theluji, maendeleo ya shughuli za barafu na theluji yamesukumwa mbele katika sehemu mbalimbali nchini China. Kwa kupitia shughuli za barafu na theluji, shughuli za utamaduni na utalii zimehimizwa zaidi katika hali ya mafungamano, na China imeanzisha njia yenye umaalumu pekee ya kuendeleza uchumi wa barafu na theluji.

“Barafu na theluji” zinatoa “matokeo ya hali joto.” Katika Mkoa wa Heilongjiang wa China, kutoka Tamasha la Taa za Barafu kwenye Bustani ya Zhaolin ya Harbin mwaka 1963, hadi kuanzishwa kwa bustani ya “Dunia ya Barafu na Theluji”, na Harbin kusifiwa kuwa maskani ya theluji unaoendeleza shughuli za utalii wa kuhifadhi mazingira ya asili, utamaduni wa barafu na theluji huko unarithishwa, na kukua katika hali ya ubunifu mpya . Baridi kali na theluji nzito zilizokuwa changamoto sasa zimekuwa msukumo mpya wa kuongeza nafasi za ajira na mapato ya watu.

Barafu na theluji vilevile ni dhahabu na fedha. Kuendeleza uchumi wa barafu na theluji nchini China, ni agizo alilotoa mara kwa mara rais Xi Jinping. Barafu na theluji si kama tu zinashirikisha kazi za sanaa na viwanda, bali pia zinaunganisha China na Dunia. Watalii wengi zaidi kutoka ndani na nje ya China wanakwenda Kaskazini Mashariki mwa China kufurahia hali ya theluji, kujiburudisha kwenye mazingira ya theluji, na kujionea uchangamfu na ukarimu wa watu wa huko. Kwenye ardhi nyeusi ya kaskazini mashariki mwa China, nguvu yake bora inaongezeka kwenye baraka na theluji, na inakaribisha siku zake za mchipuko zinazojaa uhai na matumaini zaidi.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha