Simulizi za Miji | Chaoshan, ladha freshi huamsha hisia, ngoma huamsha nafsi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 12, 2026

Kwa watu wa Eneo la Chaoshan, kila siku yao huwa inaanza na kifungua kinywa. Wakati kifuniko cha sufuria ya kuchemsha kinapofunguliwa, mvuke mweupe unajaa jikonihuku kimiminiko cha mchele kinapikwa na kutoa sauti kwenye sufuria bapa za chuma. Wateja wengi wanapenda kusimama kando ya njia mtaani, wakishika bakuli zinazotoa mvuke joto na kusifu: “Tamu sana!”

Utamaduni huu wa kifungua kinywa unakita mizizi kwenye upishi unaofanywa kwa makini kabisa juu ya vyakula vya Chaoshan vinavyozingatiwa sana “hali ya fresh” na kupikwa siku hiyo jikoni baada ya mboga au nyama kununuliwa kutoka sokoni. Ukiingia jikoni, utaona wapishi wanashirikiana kwa makini katika kufanya maandalizi ya mboga, nyama, na viungo vya aina mbalimali, na kufuatilia hali ya moto jikoni wakati wa kupika. Vyakula vya Chaoshan vinazingatia ladha asili za mboga na nyama, ambavyo upishi wake unategemea zaidiustadi wa juu wa wapishi badala ya kutumia viungo vingi.

Usiku unapofika, taa za migahawani zimewaka zaidi, sauti za ngoma zinasikika, huku ngoma ya Yingge ikichezwa. Ngoma hiyo maarufu katika eneo la Chaoshan ni mchezo wa sanaa wa kienyeji unaohusisha dansi, opera za kienyeji na mchezo wa Wushu. Katika mwaka 2006 ngoma hiyo iliorodheshwa kwenye orodha ya mali ya urithi wa kitaifa wa utamaduni usioshikika wa China. Maonesho ya Ngoma hiyo yanafanyika mara kwa mara katika sherehe za sikukuu, hafla ya matambiko na shughuli nyingine za kijadi, ambayo inaonesha hali ya shamrashamra na maombea mema.

Chaoshan inaifanya hali yake ya kufunguliwa mlango kwa kuelekea bahari ifungamane na desturi zake za maisha ya kawaida zinazofuata maadili. Vyakula vitamu vilivyopikwa kwa makini na kuwavutia watu, na maonyesho ya ngoma ya Yingge, yote hayo yanaonyesha watu wa Chaoshan wenye uaminifu, kutetea haki, kuwa na mshikamano na ushirikiano. Chaoshan lenye mafungamano ya mila na desturi na maisha ya kila siku, ikionyesha kwa dunia mambo mbalimbali na uhai wa nguvu ya utamaduni wa China katika zama tulizonazo.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha