Mwanadiplomasia Mwandamizi wa Ghana asema uhusiano kati ya China na Ghana unaendelea kuimarika

(CRI Online) Februari 13, 2026

Balozi wa zamani wa Ghana nchini China Bw. Anani Demuyakor amezisifu Ghana na China kwa kuendelea kuimarisha uhusiano wao, wa pande mbili kwa kusisitiza zaidi juu ya mabadilishano kati ya watu na watu na masuala ya maendeleo.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni na Shirika la Habari la China Xinhua, Bw. Demuyakor amesema uhusiano huo ambao tayari ni imara umepata msukumo mkubwa katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni katika sekta mbalimbali na unaendelea kuwa imara zaidi.

China ni mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Ghana na chanzo kikuu cha uwekezaji, na kwa mujibu wa takwimu kutoka Wizara ya Biashara ya China, biashara ya pande mbili ilifikia dola za Marekani bilioni 6.54 katika kipindi cha Januari-Juni 2025, ikiwakilisha ongezeko la asilimia 9.2 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha