Namibia yapokea kituo cha ardhini cha satalaiti kilichojengwa kwa msaada wa China kwa kuongeza uwezo kwenye nafasi za anga

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 13, 2026

Kituo cha Kupokea Data za Satalaiti cha Ardhini kilichojengwa kwa msaada wa China kikionekana kwenye Kituo cha Telecom Earth nje ya Windhoek, mji mkuu wa Namibia, Julai 23, 2025. (Picha imetolewa na timu ya mradi/kupitia Xinhua)

Kituo cha Kupokea Data za Satalaiti cha Ardhini kilichojengwa kwa msaada wa China kikionekana kwenye Kituo cha Telecom Earth nje ya Windhoek, mji mkuu wa Namibia, Julai 23, 2025. (Picha imetolewa na timu ya mradi/kupitia Xinhua)

WINDHOEK - Namibia imekabidhiwa rasmi Kituo cha Kupokea Data za Satalaiti cha Ardhini kilichojengwa kwa msaada wa China, huu ni mradi alama unaolenga kuongeza uwezo wa kisayansi wa nchi hiyo kwenye nafasi za anga, kukabiliana na majanga na maendeleo yanayosukumwa mbele kwa uvumbuzi wa nchi hiyo.

Kituo hicho kiko kwenye Kituo cha Telecom Earth nje ya mji mkuu, Windhoek, unatarajiwa kuiwezesha Namibia kupokea na kuchakata data za kuhisiwa kwa mbali moja kwa moja kutoka kwenye satalaiti, ikiwa ni pamoja na Satalaiti ya Maliasili za Dunia ya China na Brazil, China-Brazil Earth Resources Satellite (CBERS-4).

Akizungumza jana Alhamisi kwenye hafla ya makabidhiano hayo kwa niaba ya Rais Netumbo Nandi-Ndaitwah, Waziri Mkuu wa Namibia Elijah Ngurare ametoa shukrani kwa China kwa uungaji mkono wake huo.

"Nikiwa kwa niaba ya serikali ya Namibia na watu wa Namibia, natoa shukrani kwa Jamhuri ya Watu wa China kwa uungaji mkono wake mkubwa kupitia ujenzi wa kituo hiki cha kupokea data za satalaiti cha ardhini," Ngurare amesema.

"Hatua hii isiyo ya kawaida inaimarisha urafiki wa kudumu kati ya watu wa nchi zetu mbili na uhusiano imara wa pande mbili," ameongeza.

Ngurare amesema unngaji mkono wa kifedha na utaalamu wa tekolojia za China vimeiwezesha Namibia kujiunga na kundi teule la nchi za Afrika zenye vituo vya kisasa vya ardhini vyenye uwezo wa kupokea data za satalaiti kwa wakati halisi.

Waziri wa Elimu, Uvumbuzi, Vijana, Michezo, Sanaa na Utamaduni wa Namibia Sanet Steenkamp amekielezea kituo hicho kuwa ni hatua kubwa katika kutekeleza “Sera ya Sayansi na Teknolojia ya Anga ya Juu ya nchi ya 2021”.

Steenkamp amesema kuwa kituo hicho kitatumika kama mali ya nchi ya kimkakati, kitatoa picha zenye ubora wa hali ya juu wa utambuzi wa kipekee wa nchi yetu ili kuimarisha ufuatiliaji wa mipaka na bahari, ulinzi wa mazingira na usimamizi wa maafa.

Amesema upatikanaji wa data za satalaiti kwa wakati halisi utaboresha hatua za kukabiliana na maafa ya kimaumbile kama vile mafuriko ya maji na moto wa nyikani, ili kukwepa ucheleweshaji unaotokana na vizuizi vya kunufaika pamoja na data za kimataifa

Waziri huyo pia amezungumzia kazi kuhusu kujenga uwezo wa uendeshaji wa kituo hicho, akisema Wanamibia 14 wamekuwa wakipokea mafunzo ya kuendesha kituo hicho, na baadhi kati yao wameanza kusimamia kituo hicho na kupokea data za satalaiti.

Balozi wa China nchini Namibia Zhao Weiping amesema mradi huo unaonyesha ahadi ya China ya kuunga mkono maendeleo ya sayansi na teknolojia ya Afrika.

"Kituo cha kupokea data za satalaiti cha ardhini ni mradi wa kwanza wa maendeleo ya teknolojia ya hali ya juu uliojengwa kwa msaada wa China nchini Namibia," Zhao amesema.

Waziri Mkuu wa Namibia Elijah Ngurare (wa pili kulia, mbele) akishiriki kwenye hafla ya makabidhiano ya Kituo cha Kupokea Data za Satalaiti cha Ardhini kilichojengwa kwa msaada wa China akiwa na Balozi wa China nchini Namibia Zhao Weiping (wa pili, kushoto) kwenye Kituo cha Telecom Earth nje ya mji mkuu, Windhoek, Namibia, Februari 12, 2026. (Xinhua/Lin Jing)

Waziri Mkuu wa Namibia Elijah Ngurare (wa pili kulia, mbele) akishiriki kwenye hafla ya makabidhiano ya Kituo cha Kupokea Data za Satalaiti cha Ardhini kilichojengwa kwa msaada wa China akiwa na Balozi wa China nchini Namibia Zhao Weiping (wa pili, kushoto) kwenye Kituo cha Telecom Earth nje ya mji mkuu, Windhoek, Namibia, Februari 12, 2026. (Xinhua/Lin Jing)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha