Roboti yenye umbo wa binadamu katika Tamasha la Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China wafuaitliwa duniani

(CRI Online) Februari 19, 2026

Katika Tamasha la Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China la mwaka 2026 lililoandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG), roboti zenye umbo la binadamu zilizotengenezwa na China zimeonekana tena jukwaani, na maonesho yao yametangazwa moja kwa moja duniani kupitia Shirika la Kimataifa la Televisheni la China (CGTN), na kufuatiliwa na wanamtandao duniani kote.

Shirika la Habari la Uingereza Reuters limeripoti kuwa, uhodari wa maonesho ya roboti katika tamasha hilo umeonesha kuwa China tayari imeweka teknolojia ya roboti na AI kama kipaumbele cha mikakati yake ya kuunganisha akilibandia na utengenezaji.

Ripoti ya《India ya Leo》imesema Tamasha la Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China linalofanyika kila mwaka limekuwa “Maonesho ya Kimataifa ya Teknolojia”, ambapo roboti zenye umbo la binadamu zimecheza vitendo vigumu vya Wushu jukwaani, zikionesha maendeleo ya kasi ya China katika sekta za roboti na AI.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha