Lugha Nyingine
Zanzibar yashirikiana na kampuni binafsi kwa mpango wa dola za kimarekani milioni 12 wa kurejesha urithi wa mabaki ya kitamaduni
Serikali ya Zanzibar imezindua mpango wa dola za kimarekani milioni 12 wa kurejesha urithi wa mabaki ya kitamaduni kwa kushirikiana na kampuni binafsi ya Infinity Developments ili kuimarisha uhifadhi wa utamaduni na kuongeza mvuto wa utalii.
Mpango huo unalenga kurejesha na kuboresha maeneo kadhaa ya kihistoria katika visiwa hivyo, yakiwemo maeneo ya ndani na nje ya Mji Mkongwe, eneo la urithi wa dunia wa UNESCO.
Maofisa walisema mradi huo ni ushirikiano muhimu wa serikali na sekta binafsi, unaoweka uhifadhi wa utamaduni kuwa kipaumbele cha maendeleo ya kiuchumi ya muda mrefu.
Mpango wa kurejesha vivutio utashughulikia sehemu muhimu kama vile Ngome Kongwe, Jumba la Makumbusho la Mahakama Kuu, na majengo kadhaa ya kihistoria. Kazi zilizopangwa ni pamoja na uhifadhi wa miundo, uboreshaji wa miundombinu, na uboreshaji wa vifaa vya wageni na mipango ya kitamaduni.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



