Lugha Nyingine
China yatoa wito wa suluhisho la kudumu na lenye ufanisi la mgogoro wa Sudan
Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Fu Cong, ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuheshimu mkataba wenye mapendekezo matano katika jitihada zake za pamoja kutafuta suluhisho la kudumu na lenye ufanisi la mgogoro wa Sudan, ambao umeleta mateso makubwa kwa nchi hiyo na watu wake.
Akiongea kwenye mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu suala la Sudan, balozi Fu amesema jumuiya ya kimataifa haiwezi kuruhusu mgogoro wa Sudan uendelee kuenea, na wala haiwezi kukubali kuwepo kwa vifo zaidi vya raia.
Mkataba wa vipengele vitano unajumuisha kufikiwa makubaliano ya kukomesha mapigano haraka iwezekanavyo; kupunguza msukosuko wa kibinadamu; kuimarisha juhudi za upatanishi; umiliki wa Sudan; na makubaliano ya kuunganisha maendeleo na usalama.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



