Lugha Nyingine
Wang Yi asema mstari mwekundu kuhusu kulinda raia katika migogoro haupaswi kuvukwa
BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi kwenye mazungumzo kwa njia ya simu na Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan, naibu waziri mkuu ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa Falme za Kiarabu (UAE) jana Jumatano amesema kwamba mstari mwekundu kuhusu kulinda raia katika migogoro haupaswi kuvukwa.
Abdullah amemwelezea Wang juu ya hali ya kikanda na msimamo wa UAE, akisema nchi hiyo si upande katika vita hivyo, haijashiriki katika mgogoro wa sasa, na haipaswi kufanyiwa mashambulizi haramu.
Ameeleza shukrani kwa msimamo usioyumbayumba wa China wa kutopendelea na kuegemea upande wowote, akiongeza kuwa UAE inatarajia China kuendelea kubeba jukumu la kivitendo na muhimu chini ya hali mbaya ya sasa ili kuzuia kupamba moto zaidi kwa mivutano ya kikanda.
"UAE itaendelea kuchukua hatua za kuhakikisha usalama wa wafanyakazi na taasisi za China nchini," Abdullah amesema.
Kwa upande wake, Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesisitiza msimamo wa China juu ya hali ya sasa nchini Iran, akisema kuwa kuenea kwa vita hakunufaishi maslahi ya yeyote na kwamba watu wa eneo hilo ndio watakaoteseka.
Amesisitiza kwamba malengo yasiyo ya kijeshi yanayohusiana na nishati, uchumi na shughuli za watu kujipatia vipato hayapaswi kushambuliwa, na kwamba usalama wa njia za meli lazima ulindwe.
Wang amesema kuwa UAE ilikuwa imefanya kazi kwa ajili ya amani hata kabla ya mgogoro huo kuzuka, na kwamba mkutano wa hivi karibuni wa mawaziri wa mambo ya nje wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ulisisitiza kwamba mazungumzo na diplomasia ndiyo njia pekee ya kushinda mgogoro huo wa sasa na kulinda usalama wa kikanda, ambao China inayathamini.
“China inaunga mkono madai halali ya UAE ya kulinda usalama wake wa taifa na inaunga mkono nchi za kikanda katika juhudi zao zinazoendelea za kutatua mizozo kupitia njia za kidiplomasia,” Wang amesema.
“China haitaikatia tamaa amani na itaendelea kubeba jukumu la kiujenzi,” Wang amesema, akiongeza kuwa China itatuma mjumbe wake maalum juu ya suala la Mashariki ya Kati katika eneo hilo ili kufanya juhudi za upatanishi ili kulirudisha eneo hilo kwenye amani na utulivu.
Wang pia ameelezea matumaini kwamba UAE itaendelea kuhakikisha usalama wa raia na taasisi za China nchini humo.

Kupatwa kwa mwezi kikamilifu kwashuhudiwa katika sehemu mbalimbali nchini China

"Tamasha la Maolong" la kabila la Wayilao lasherehekewa kwa ngoma ya dragoni mkoani Guizhou, China

Mji mkongwe wa Wuzhen, China wazindua shughuli mbalimbali wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China

Hong Kong Yasherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa Farasi wa China kwa Maonyesho ya Fataki
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma