Lugha Nyingine
Tume ya utendaji wa mkutano yachaguliwa, na ajenda za mkutano wa Bunge la Umma la China zapitishwa

Zhao Leji, mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge la Umma la China akiongoza kikao cha maandalizi ya mkutano wa nne wa Bunge hilo la 14 kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing Machi 4, 2026. (Xinhua/Shen Hong)
BEIJING – Wajumbe wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) wamekusanyika Beijing jana Jumatano kwenye kikao cha maandalizi ya mkutano wa mwaka wa bunge hilo, ambapo wamechagua wajumbe wa tume ya utendaji wa mkutano wa mwaka na kupitisha ajenda za mkutano huo uliopangwa kuanza leo Alhamisi.
Zhao Leji, mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge la Umma la China aliongoza kikao cha maandalizi. Amesema, kazi zote za maandalizi ya mkutano wa nne wa mwaka zimekamilika.
Wajumbe 167 wa mkutano wamechaguliwa kuwa wajumbe wa Tume ya utendaji wa mkutano wa mwaka, na Li Hongzhong atakuwa katibu mkuu wa mkutano huo.
Kikao hicho cha maandalizi pia kimepitisha ajenda za mkutano huo wa mwaka. Ajenda hizo zinahusu kujadili na kupitisha ripoti ya kazi ya serikali, kuthibitisha Mswada wa Mpango wa 15 wa Maendeleo ya Uchumi na Jamii wa Miaka Mitano (2026-2030), kuthibitisha ripoti kuhusu utekelezaji wa mpango wa mwaka 2025 wa maendeleo ya uchumi na jamii na ripoti kuhusu mswada wa mpango wa mwaka 2026, pamoja na mswada wa mpango wa maendeleo ya uchumi na jamii wa mwaka 2026.
Baada ya kumalizika kwa kikao cha maandalizi, Tume ya utendaji wa mkutano wa mwaka ulifanya mkutano, ukiamua ratiba ya mkutano huo wa mwaka wa Bunge la Umma na mambo mengine. Bunge la Umma la China litafanya mkutano wake wa mwaka huu kuanzia Tarehe 5 hadi Tarehe 12 Machi mwezi huu.
Kabla ya kikao hicho cha maandalizi, Baraza la Wenyeviti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China lilifanya mkutano kuhusu kazi ya maandalizi ya mkutano wa mwaka.
Vikao hivyo vya tume ya utendaji na Baraza la Wenyeviti vyote viliongozwa na Zhao.

Zhao Leji, mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge la Umma la China akiongoza kikao cha kwanza cha tume ya utendaji ya mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing Machi 4, 2026. (Xinhua/Ding Haitao)

Zhao Leji, mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge la Umma la China akiongoza kikao cha 64 cha Baraza la Wenyeviti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la 14 la Umma kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 4, 2026. (Xinhua/Rao Aimin)

Kupatwa kwa mwezi kikamilifu kwashuhudiwa katika sehemu mbalimbali nchini China

"Tamasha la Maolong" la kabila la Wayilao lasherehekewa kwa ngoma ya dragoni mkoani Guizhou, China

Mji mkongwe wa Wuzhen, China wazindua shughuli mbalimbali wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China

Hong Kong Yasherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa Farasi wa China kwa Maonyesho ya Fataki
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma