Lugha Nyingine
Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China laanza mkutano wa mwaka

Mkutano wa nne wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) ukifunguliwa katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 4, 2026. (Xinhua/Yan Yan)
BEIJING - Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), chombo cha juu cha mashauri ya kisiasa cha China, imefanya mkutano wake wa nne wa mwaka kuanzia jana Jumatano mjini Beijing ambapo Rais Xi Jinping na viongozi wengine wa Chama na serikali, wakiwemo Li Qiang, Zhao Leji, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng, walihudhuria kwenye ufunguzi wa mkutano huo katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.
Ajenda za mkutano huo zilithibitishwa na kupitishwa kwenye ufunguzi.
Wakati wa mkutano huo, washauri wa kisiasa zaidi ya 2,000 watafanya mashauriano na majadiliano ya kina na kutoa maoni na mapendekezo yao, ambapo wakifuata maamuzi na mipango ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) wataweka mkazo katika kufuatilia utungaji na utekelezaji wa mwongozo wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano.
Wang Huning, mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China, alitoa ripoti ya kazi kwa niaba ya Kamati ya Kudumu ya baraza hilo kwenye mkutano huo wa kufunguliwa.
Wang alikumbuka kazi ya baraza hilo katika mwaka uliopita. Amesema baraza hilo na Kamati yake ya Kudumu vimechukulia uongozi wa CPC, umoja wa mstari wa mbele na demokrasia ya mashauriano kuwa msingi mkuu mzima, vikiunganisha kazi zao na majukumu makuu ya Chama na nchi, na vimeonesha vya kutosha umuhimu wa chombo maalum cha mashauriano.
Akitazama siku za baadaye katika mwaka 2026, amewahimiza wajumbe wa baraza hilo kuhamasisha uungaji mkono wa umma, kujenga maoni ya pamoja zaidi, na kukusanya hekima na nguvu kwa ajili ya mwanzo mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano.
Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China linafanya kazi muhimu katika ushirikiano wa vyama vingi na mashauriano ya kisiasa chini ya uongozi wa CPC. Wajumbe wake wanatoka katika vyama mbalimbali vya kisiasa, mashirika ya umma, watu wasio na vyama na sekta mbalimbali za jamii.
Mkutano huo pia umetoa ripoti kuhusu hali ya kushughulikia mapendekezo yaliyowasilishwa na washauri wa kisiasa tangu mkutano uliopita wa tatu wa mwaka wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya CPPCC uliofanyika mwezi Machi 2025.
Kamati ya Kitaifa ya CPPCC ilipokea mapendekezo 5,992 kutoka kwa wajumbe wake katika mwaka uliopita, ambapo 5,061 yalikubaliwa na kufanyiwa kazi. Kiwango cha kufanyiwa kazi kwa mapendekezo yaliyokubaliwa kilifikia asilimia 99.9.

Mkutano wa nne wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) ukifunguliwa kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing Machi 4, 2026. (Xinhua/Liu Bin)

Mkutano wa nne wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) ukifunguliwa kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing Machi 4, 2026. (Xinhua/Liu Bin)

Wang Huning, mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), akitoa ripoti ya kazi kwa niaba ya Kamati ya Kudumu ya kamati ya hiyo ya kitaifa kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya CPPCC katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 4, 2026. (Xinhua/Yao Dawei)

Shi Taifeng akiongoza ufunguzi wa mkutano wa nne wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing Machi 4, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)

He Baoxiang akiwa kwa niaba ya Kamati ya Kudumu ya kamati ya kitaifa ya CPPCC alitoa hotuba kuhusu hali ya kushughulikia mapendekezo kutoka kwa washauri wa kisiasa tangu mkutano wa tatu wa kamati ya kitaifa ya 14 ya CPPCC kwenye mkutano wa nne wa kamati hiyo ya kitaifa ya 14 uliofunguliwa katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing Machi 4, 2026. (Xinhua/Liu Weibing)

Mkutano wa nne wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) ukifunguliwa katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing Machi 4, 2026. (Xinhua/Yao Dawei)

Kupatwa kwa mwezi kikamilifu kwashuhudiwa katika sehemu mbalimbali nchini China

"Tamasha la Maolong" la kabila la Wayilao lasherehekewa kwa ngoma ya dragoni mkoani Guizhou, China

Mji mkongwe wa Wuzhen, China wazindua shughuli mbalimbali wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China

Hong Kong Yasherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa Farasi wa China kwa Maonyesho ya Fataki
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma