Bunge la Umma la China lafungua mkutano wa mwaka

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 05, 2026

Kikao cha kufungua mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) kikifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Machi 5, 2026. (Xinhua/Wang Ye)

BEIJING - Bunge la 14 la Umma la China, chombo cha juu cha utungaji sheria cha China, limefungua mkutano wake wa nne leo Alhamisi asubuhi kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.

Xi Jinping na viongozi wengine wa Chama na serikali wamehudhuria kikao hicho cha kufungua.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang ametoa ripoti ya kazi ya serikali kwenye kikao hicho.

Wajumbe wamethibitisha mswada wa mwongozo wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030) wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya China.

Wamethibitisha ripoti juu ya utekelezaji wa mpango wa mwaka 2025 kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya China na ripoti juu ya mswada wa mpango wa mwaka 2026, na mswada wa mpango wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii China katika mwaka 2026.

Wajumbe pia wamethibitisha ripoti juu ya utekelezaji wa bajeti za serikali kuu na serikali za mitaa kwa mwaka 2025 na ripoti juu ya mswada wa bajeti za serikali kuu na serikali za mitaa kwa mwaka 2026, na mswada ya bajeti za serikali kuu na serikali za mitaa kwa mwaka 2026.

Li Hongzhong, makamu mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, alitoa hotuba ya maelezo juu ya mswada wa kanuni za mazingira, mswada wa sheria kuhusu kuhimiza umoja na maendeleo ya makabila, na mswada wa sheria kuhusu mipango ya maendeleo ya kitaifa, mtawalia.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akitoa ripoti ya kazi ya serikali katika kikao cha kufungua mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Machi 5, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)

Zhao Leji akiongoza kikao cha kufungua mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Machi 5, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

Li Hongzhong, makamu wa mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, akitoa hotuba ya maelezo juu ya mswada wa kanuni za mazingira, mswada wa sheria kuhusu kuhimiza umoja na maendeleo ya makabila, na mswada wa sheria kuhusu mipango ya maendeleo ya kitaifa katika kikao cha kufungua mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Machi 5, 2026. (Xinhua/Ding Haitao)

Kikao cha kufungua mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) kikifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Machi 5, 2026. (Xinhua/Ding Haitao)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha