Lugha Nyingine
Seneti ya Marekani yashindwa kusukuma mbele azimio la mamlaka ya vita lenye lengo la kudhibiti operesheni za kijeshi za Trump za Iran
Picha hii iliyopigwa Novemba 5, 2025 ikionyesha jengo la Bunge la Marekani, Capitol mjini Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Hu Yousong)
WASHINGTON – Baraza la Seneti la Bunge la Marekani limeshindwa kusukuma mbele azimio la mamlaka ya vita lenye kulenga kudhibiti operesheni za kijeshi za Rais wa Marekani Donald Trump dhidi ya Iran, huku wabunge wa vyama vya Democrat na Republican wakiendelea kuwa wamegawanyika vikali kuhusu suala hilo.
Kwa kura 53 za hapana na 47 za ndiyo, baraza hilo la juu linaloongozwa na wabunge wa Chama cha Republican limezuia azimio hilo, ambalo lililenga kumzuia Trump kuamrisha mashambulizi zaidi ya kijeshi dhidi ya Iran bila idhini ya bunge.
Kwenye hotuba ya kipindi cha majadiliano kabla ya kupigwa kura hiyo, wabunge wa Democrat wamekosoa kwa kiasi kikubwa mashambulizi hayo ya kijeshi dhidi ya Iran wakati huohuo wabunge wa Republican wamemtetea rais kwa kiasi kikubwa.
Mbunge wa chama cha Democrat na askari mstaafu Tim Kaine, ambaye alianzisha hatua hiyo, amesema kwamba "utawala na seti za sababu zao zinazobadilikabadilika, na hata kwenye mazingira ya siri, hazikuweza kutoa ushahidi wowote, kwamba Marekani ilikuwa chini ya tishio la shambulizi kutoka Iran."
"Je, hatujajifunza chochote kutokana na miaka 25 ya vita katika Mashariki ya Kati? Wanajeshi na wakandarasi wa kijeshi 14,000 wa Marekani waliuawa nchini Iraq na Afghanistan ... mamia kwa maelfu ya vifo vya raia ... nchini Iraq na Afghanistan, zaidi ya trilioni 8 zilizotumika ambazo zingeweza kutumika katika huduma ya afya ya Marekani, kwenye nyumba za makazi za Marekani, kwenye elimu ya Marekani, zilizotumika kwenye vita nchini Afghanistan na Iraq. Na tulipata nini kwa hilo?" amehoji Kaine.
Mbunge wa chama cha Democrat Patty Murray, ambaye ni makamu mwenyekiti wa Kamati ya Matumizi ya Fedha ya Seneti, amesema "hatupaswi kucheza kamari maisha ya Wamarekani kwa mipango isiyokamilika, malengo yasiyoeleweka na mustakabali usio na uhakika kabisa."
Wabunge wa Republican wamesema kwamba hatua hizo za Trump nchini Iran zilikuwa muhimu na zenye sababu, wakiwashutumu wabunge wa Democrat kwa kupinga hatua hizo kwa sababu za kichama.

Kupatwa kwa mwezi kikamilifu kwashuhudiwa katika sehemu mbalimbali nchini China

"Tamasha la Maolong" la kabila la Wayilao lasherehekewa kwa ngoma ya dragoni mkoani Guizhou, China

Mji mkongwe wa Wuzhen, China wazindua shughuli mbalimbali wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China

Hong Kong Yasherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa Farasi wa China kwa Maonyesho ya Fataki
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma