Lugha Nyingine
Rais wa Afrika Kusini atoa wito wa usalama na matumizi ya nishati mbalimbali kutokana na msukosuko duniani

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akizungumza kwenye Mkutano wa Nishati wa Afrika 2026 (Africa Energy Indaba 2026) mjini Cape Town, Afrika Kusini, Machi 4, 2026. (Picha na Xabiso Mkhabela/Xinhua)
CAPE TOWN - Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametoa wito wa uunganishaji zaidi wa nishati katika Bara la Afrika ili kuimarisha usalama na kuwa na matumizi ya nishati mbalimbali kwa bara hilo kutokana na masoko duniani kukabiliwa na msukomsuko mkubwa.
Akizungumza jana Jumatano kwenye Mkutano wa Nishati wa Afrika 2026 (Africa Energy Indaba 2026) mjini Cape Town, Ramaphosa amesema mivutano inayozidi kupamba moto ya siasa za kijiografia na kutatizika kwa mnyororo wa usambazaji vimeongeza hatari kwa uchumi wa nchi za Afrika unaotegemea usambazaji wa nishati kutoka nje.
"Afrika tayari inakabiliwa na athari za mgogoro unaozidi kupamba moto katika eneo la Mashariki ya Kati, na matatizo kwenye minyororo ya usambazaji na bei za juu za nishati," amesema, akisema kuwa mazingira ya siasa za kijiografia kama hayo yanayobadilika "yanasisitiza udhaifu wa nchi zenye uchumi unaotegemea uagizaji kutoka nje kote Afrika."
Rais Ramaphosa amezihimiza nchi za Afrika kuharakisha uundaji wa mfumo uliounganishwa wa nishati wenye uwezo wa kusambaza umeme kuvuka mipaka na kusawazisha rasilimali mbalimbali, zikiwemo za umeme unaotokana na maji, jua, upepo na gesi. Amesema, gridi iliyounganishwa, inaweza kuimarisha gharama nafuu, uhakika na uwezo wa ushindani wa viwanda.
"Kazi sasa ni kujenga aina tofauti ya mfumo wa nishati, ambao unaiunganisha Afrika na yenyewe na ambao unaruhusu uchumi wetu kukua kwa pamoja badala ya kutengana," Ramaphosa amesema.
“Licha ya mafuta, gesi, rasilimali za nishati mbadala na madini muhimu kupatikana kwa wingi, Waafrika zaidi ya milioni 600 bado wanakosa huduma ya umeme,” Amesema, akiuelezea umaskini wa nishati kuwa ni kizuizi cha maendeleo ya viwanda na uwekezaji.
Ukiwa umefanyika kuanzia Jumanne hadi leo Alhamisi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Cape Town chini ya kaulimbiu ya "Kuwasha Mapinduzi ya Umemeu," mkutano huo wa 18 wa nishati wa Afrika umekusanya wajumbe zaidi ya 1,600 kutoka nchi 37 za Afrika, wakiwemo mawaziri 15 wa nishati, pamoja na wawekezaji, wasimamizi na watendaji wa sekta hiyo wanaotaka kuharakisha kuendana kwa miundombinu na uhamasishaji wa uwekezaji.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akizungumza kwenye Mkutano wa Nishati wa Afrika 2026 (Africa Energy Indaba 2026) mjini Cape Town, Afrika Kusini, Machi 4, 2026. (Picha na Xabiso Mkhabela/Xinhua)

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akizungumza kwenye Mkutano wa Nishati wa Afrika 2026 (Africa Energy Indaba 2026) mjini Cape Town, Afrika Kusini, Machi 4, 2026. (Picha na Xabiso Mkhabela/Xinhua)

Kupatwa kwa mwezi kikamilifu kwashuhudiwa katika sehemu mbalimbali nchini China

"Tamasha la Maolong" la kabila la Wayilao lasherehekewa kwa ngoma ya dragoni mkoani Guizhou, China

Mji mkongwe wa Wuzhen, China wazindua shughuli mbalimbali wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China

Hong Kong Yasherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa Farasi wa China kwa Maonyesho ya Fataki
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma