Watu zaidi ya 200 wafariki kufuatia maporomoko ya ardhi katika eneo la uchimbaji madini mashariki mwa DRC

(CRI Online) Machi 05, 2026

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imesema, idadi ya watu waliofariki kufuatia maporomoko makubwa ya ardhi yaliyotokea Jumanne wiki hii kwenye eneo la uchimbaji madini ya coltan huko Rubaya, Jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa nchi hiyo imefikia watu zaidi ya 200 wakiwemo watoto 70.

Awali, iliripotiwa juzi Jumanne kuwa, watu 7 walikuwa wamefariki katika ajali hiyo huku wengine wakiwa hawajulikani walipo.

Taarifa hiyo ya hivi punde ya Wizara ya Madini ya DRC iliyotolewa jana Jumatano imesema kuwa maporomoko hayo yalisababishwa na mvua kubwa iliyonyesha siku hiyo, na kufukia njia kadhaa za kuingia migodini.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha