MWC 2026 wahitimishwa nchini Hispania, ukionesha namna AI inavyobadilisha sekta ya mawasiliano ya simu (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 06, 2026
MWC 2026 wahitimishwa nchini Hispania, ukionesha namna AI inavyobadilisha sekta ya mawasiliano ya simu
Watu wakitembelea Mkutano wa Dunia wa Simu 2026 (MWC) mjini Barcelona, Hispania, Machi 5, 2026. (Xinhua/Cheng Min)

BARCELONA – Mkutano wa Dunia wa Simu 2026 (MWC) umehitimishwa jana Alhamisi mjini Barcelona, Hispania, ukiwa umeonesha namna ongezeko kubwa la AI linavyosukuma mawasiliano ya simu kuendelea kuzidi kuwa muunganisho wa msingi na kuelekea mfumo mpana zaidi wa kidijitali unaojumuisha kompyuta ya wingu, majukwaa ya data na matumizi kiviwanda.

Mkutano huo wa nne, uliofanyika chini ya kaulimbiu ya "Zama ya IQ," uliwaleta pamoja wahudhuriaji zaidi ya 100,000 kutoka nchi na maeneo 207, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa Alhamisi na mratibu GSMA.

Mkutano wa mwaka huu ambao umeadhimisha miaka 20 ya kuwepo kwa tukio hilo mjini Barcelona, pia ulivutia waonyeshaji bidhaa, wafadhili na washirika takribani 2,900, zikiwemo kampuni zaidi ya 350 kutoka China, mratibu huyo ameeleza.

Katika mkutano huo wa mwaka huu, inatambulika sana kwamba kadri AI inavyohama kutoka dhana hadi matumizi ya kiwango kikubwa, mitandao ya simu inahama kutoka miundombinu ya msingi ya muunganisho hadi majukwaa yanayounga mkono programu zinazoendeshwa na AI.

Peter Jarich, mkuu wa GSMA Intelligence, amesema katika kikao cha mwisho cha mkutano huo kwamba, mkutano wa mwaka huu umeonyesha kuwa sekta ya mawasiliano ya simu inaingia katika awamu mpya ya maendeleo, huku mkazo ukibadilika kutoka kuboresha ufanisi wa mtandao hadi kujenga usanifu wa mawasiliano ulio wazi zaidi na mifumo ya ikolojia inayohusiana na AI, kompyuta ya wingu na majukwaa ya data.

Kuanzia uvumbuzi unaowezeshwa na AI, ikiwemo simu ya roboti, hadi programu za AI zilizojengwa kwenye mifumo ya AI ya Huawei na majukwaa ya kompyuta, kama vile programu ya kisasa ya kusaidia uwekezaji ya kampuni ya YSSTech iliyoundwa kwa ajili ya kufanya uchambuzi wa biashara na kutoa uungaji mkono wa kufanya maamuzi, teknolojia mbalimbali za China zimeibuka kuwa chombo muhimu kwenye maonyesho.

Zaidi ya hayo, kampuni za China zimeshinda tuzo nyingi katika kategoria mbalimbali zikiwemo za miundombinu ya mtandao, bidhaa za kivumbuzi na za suluhu za sekta katika Tuzo za Global Mobile (GLOMO).

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha