UNESCO yaelezea wasiwasi juu ya uharibifu wa maeneo ya urithi wa dunia nchini Iran (2)

(CRI Online) Machi 06, 2026
UNESCO yaelezea wasiwasi juu ya uharibifu wa maeneo ya urithi wa dunia nchini Iran
Picha hii ya kumbukumbu iliyopigwa Desemba 12, 2022 ikionyesha Jumba la Golestan mjini Tehran, mji mkuu wa Iran. (Xinhua)

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limeeleza wasiwasi wake juu ya ulinzi wa maeneo ya urithi wa kitamaduni katika eneo la Mashariki ya Kati, hasa uharibifu wa maeneo ya Urithi wa Dunia mjini Tehran, mji mkuu wa Iran, wakati huu ambapo migogoro ikizidi kupamba moto katika eneo la Mashariki ya Kati.

Taarifa iliyotolewa Jumanne wiki hii na UNESCO imerejea ripoti kwamba Jumba la Ghoulestan (pia linalojulikana kwa jina la "Jumba la Rose") eneo la Urithi wa Dunia la UNESCO mjini Tehran limeharibiwa katika mitikisiko ya shambulizi la anga.

UNESCO imesema inafuatilia kwa karibu hali ya urithi wa kitamaduni nchini Iran na katika eneo la Mashariki ya Kati ili kuhakikisha ulinzi wake.

Pia UNESCO imesema imewafahamisha wahusika kuhusu uratibu wa kijiografia wa maeneo ya Urithi wa Dunia na maeneo yenye umuhimu wa kitaifa ili kuzuia uharibifu wowote unaoweza kutokea.

Shirika hilo limesisitiza kwamba, mali ya kitamaduni inalindwa chini ya sheria za kimataifa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha