Lugha Nyingine
Mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege uliofadhiliwa na China wachangia ongezeko la idadi ya abiria nchini Zimbabwe (4)
![]() |
| Watu wakipitia utaratibu wa forodha kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe, Harare, Zimbabwe, Machi 5, 2026. (Picha na Tafara Mugwara/Xinhua) |
HARARE - Kampuni ya Viwanja vya Ndege ya Zimbabwe (ACZ) imesema kuwa, idadi ya abiria kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe wa Zimbabwe imeongezeka na inakadiriwa kufikia takriban milioni 1.65 katika mwaka 2025, hasa kufuatia mradi wa upanuzi uliofadhiliwa na China uliozinduliwa mwaka 2023.
Mtendaji Mkuu wa ACZ Tawanda Gusha ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwenye mahojiano ya hivi karibuni kwamba nchi hiyo inafurahia sana mradi huo wa kisasa uliofadhiliwa na Benki ya Export-Import ya China (China EximBank), ambao umeonesha umuhimu wake mkubwa katika ongezeko la idadi ya abiria.
"Tumeona idadi ya abiria iliyoongezeka kwenye uwanja wa ndege, na pia tumepokea maoni mengi chanya kutoka kwa watumiaji wa uwanja wa ndege," Gusha amesema. "Tunafurahi sana kuhusu hilo, na tunafurahi sana pia kupata fursa hiyo."
Mradi huo uliotekelezwa na kampuni ya Kimataifa ya Jiangsu ya China, ulihusisha ujenzi wa kituo kipya cha abiria wa kimataifa, mageti mapya ya kupandia ndege na madaraja ya ndege, pamoja na mifumo ya mawasiliano ya habari na zana na majengo mengine vinavyohusika ambavyo vyote vimeboreshwa kwa ngazi ya juu.
Akivielezea zana na majengo hayo kuwa ni "vya kisasa zaidi," Gusha amesema uwanja huo wa ndege umewafanya "wajivunie sana," na wanapanga kushindana katika tuzo za kimataifa ili kuonyesha miundombinu yake ya kisasa na huduma nzuri sana zenye ubora.
Amesema kuwa, mradi huo umesukuma mbele kwa udhahiri sekta ya usafiri wa ndege ya Zimbabwe na utaisaidia serikali ya Zimbabwe kufikia malengo yake ya Matarajio ya Mwaka 2030.
"Nafurahia kuambiwa mradi huu umefanya kazi yake ya kuhimiza juhudi katika kung'arisha Sura ya Zimbabwe duniani na kuboresha mazingira yake ya biashara," amesema Ban Yongzhi, mwakilishi mkuu wa Benki ya Exim ya China katika ofisi ya kusini-mashariki mwa Afrika.
Ban ameliambia Xinhua kwamba benki hiyo ya China imesaidia kutekeleza miradi mbalimbali ya alama katika nchi mbalimbali za Afrika katika miaka mingi iliyopita, ikiwa na matumaini ya kusukuma mbele maendeleo ya bara la Afrika na kuboresha maisha ya watu.
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe ni uwanja mkubwa zaidi nchini Zimbabwe, ukitumika kama lango muhimu linalounganisha Harare, mji mkuu wa nchi hiyo, na maeneo ya kikanda na kimataifa.

Sikukuu ya Jadi ya Taa ya China yasherehekea mkoani Zhejiang

Kupatwa kwa mwezi kikamilifu kwashuhudiwa katika sehemu mbalimbali nchini China

"Tamasha la Maolong" la kabila la Wayilao lasherehekewa kwa ngoma ya dragoni mkoani Guizhou, China

Mji mkongwe wa Wuzhen, China wazindua shughuli mbalimbali wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
