Ujumbe wa Umoja wa Mataifa walaani matumizi ya droni mashariki mwa DRC (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 12, 2026
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa walaani matumizi ya droni mashariki mwa DRC
Wafanyakazi wakikagua hali ya uharibifu baada ya shambulio la droni mjini Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Machi 11, 2026. (Str/Xinhua)

GOMA - Ujumbe wa Shirika la Umoja wa Mataifa wa Kuleta Utulivu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) umelaani matumizi ya droni huko Goma, mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kaskazini jana Jumatano.

Milipuko ilisikika jana Jumatano asubuhi katika mji huo, ambapo kundi la waasi la Vuguvugu ya Machi 23 (M23) lilisema vikosi vya jeshi la serikali ya DRC lingebeba lawama juu ya shambulizi hilo.

Takwimu za vifo vya watu zilizotolewa na M23 zimeonesha kuwa, watu watatu wameuawa, akiwemo raia wa Ufaransa aliyefanya kazi katika Shirika la Mfuko wa Watoto la Umoja wa Mataifa.

Mashuhuda kadhaa wameripoti kwamba mabomu yalirushwa wakati wa asubuhi, majira ya saa 10 alfajiri kwa saa za DRC, na kusababisha milipuko mikubwa katika baadhi ya maeneo ya wakazi wa mji huo.

Serikali ya DRC haijatoa taarifa yoyote mara moja kuhusu hilo.

Mji wa Goma ni kituo kikubwa cha mawasiliano na usambazaji wa bidhaa cha kikanda, mji huo umekuwa chini ya udhibiti wa waasi wa M23 tangu mwishoni mwa Januari 2025.

Vyombo vya habari vya DRC vimeripoti kuwa, mapigano yamekuwa yakipamba moto katika wiki za hivi karibuni kwenye medani kadhaa za mapigano kati ya vikosi vya serikali ya DRC na waasi wa M23 katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha