Lugha Nyingine
Huduma ya treni ya usafiri wa abiria wa kimataifa yaunganisha China na DPRK (5)
SHENYANG - Treni ya usafiri wa abiria wa kimataifa inayounganisha Mji wa Dandong katika Mkoa wa Liaoning, kaskazini mashariki mwa China na Mji wa Pyongyang, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu ya Korea (DPRK), imeanza kutoa huduma rasmi jana Alhamisi.
Treni hiyo yenye mabehewa matano ya abiria, iliondoka kutoka mji wa mpakani wa Dandong saa 4 asubuhi (Saa za Beijing) na ilikuwa imepangwa kuwasili Pyongyang majira ya saa 12:07 jioni kwa saa za Pyongyang.
Kwenye ukumbi wa abiria wa kimataifa wanaoondoka katika stesheni ya reli ya Dandong, ratiba za treni, skrini za kielektroniki na kaunta za huduma zilionyesha maandishi kwa lugha zote mbili za Kikorea na Kichina.
"Nimefurahi sana kurudi nyumbani kwa treni leo," amesema abiria wa DPRK, ambaye alinunua tiketi yake siku ya Jumatano baada ya kuambiwa kuwepo kwa huduma hiyo.
Song Ping, mfanyakazi wa kituo cha ukaguzi wa kuingia na kutoka cha mpaka wa Dandong, amesema mamlaka zimechukua hatua za kuhakikisha uidhinishaji rahisi wa kupitia ukaguzi katika siku ya kwanza ya uendeshaji wa treni. Amesema, mchakato wa ukaguzi wa treni nzima umefupishwa kuwa wa ndani ya dakika 30.
Treni za usafiri wa abiria zinaendeshwa kila siku katika nchi hizo mbili kwa mwelekeo wa kila upande. Treni inayoondoka kutoka Pyongyang inaondoka saa 4:26 asubuhi kwa saa za Pyongyang na imepangwa kuwa ikifika Dandong saa 10:23 jioni (Saa za Beijing).
Mtendaji wa ofisi ya mambo ya kimataifa ya kampuni ya Kundi la Reli la China amesema huduma hiyo ya treni itatumika kama dirisha muhimu kwa wasafiri wa kuvuka mpaka na kiunganishi cha kuimarisha urafiki kati ya nchi hizo mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




