Lugha Nyingine
Meli kubwa ya utalii ya pili ya kuundwa nchini China kukabidhiwa ifikapo mwishoni mwa mwaka (5)
![]() |
| Picha iliyopigwa Machi 16, 2026 ikionesha muonekano wa meli kubwa ya utalii “Adora Flora City” huko Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua/Ding Ting) |
Meli kubwa ya utalii ya pili ya kuundwa nchini China inatarajiwa kukabidhiwa ifikapo mwishoni mwa mwaka 2026, huku utengenezaji wa muundo wake mkuu ukiwa umekamilika, kwa mujibu wa muundaji wa meli hiyo, Shirika la Ujenzi wa Meli la China (CSSC).
Meli hiyo kubwa ya utalii, Adora Flora City, imepangwa kuondolewa gatini Machi 20 kwa ajili ya hatua inayofuata ya majaribio ya kutia nanga kwenye gati (dockside mooring), na majaribio ya baharini yamepangwa kufanyika mwishoni mwa Mei, amesema muundaji huyo.
Ikiwa na uwezo wa jumla wa nafasi zake kushikilia uzito wa tani 141,900 (Gross Volume), meli hiyo inawakilisha hatua zaidi kwenda mbele katika uwezo wa China wa kuunda meli kubwa za utalii.
Ikilinganishwa na meli kubwa ya utalii ya kwanza kuundwa nchini China, Adora Magic City, meli hiyo mpya ina mfululizo wa maboresho ya usanifu na ujenzi. Kampuni ya CSSC imesema, meli hiyo ina urefu wa mita 17.4 zaidi, inatoa maeneo mapana zaidi ya umma na huduma nzuri zaidi za ndani zilizoboreshwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




