Lugha Nyingine
Jukwaa la vyombo vya habari la China na DRC lahimiza kunufaishana na ushirikiano wenye mafanikio kwa pande zote (3)
KINSHASA - Jukwaa la Vyombo vya Habari la China na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) chini ya kaulimbiu ya "Mambo ya Kisasa ya China na Njia ya Maendeleo ya DRC: Kuchunguza kwa Pamoja Njia Mpya kwa ajili ya Kunufaishana na Ushirikiano wenye Mafanikio kwa Pande Zote," limefanyika jana Jumatano mjini Kinshasa, mji mkuu wa DRC.
Jukwaa hilo limevutia wanasiasa, wawakilishi wa vyombo vya habari na viongozi wa kibiashara wapatao 250 kutoka nchi zote mbili.
Katika hotuba kwa njia ya video kwenye hafla ya ufunguzi, Fu Hua, Mkuu wa Shirika la Habari la China, Xinhua, amesisitiza kwamba mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na mataifa ya Afrika, vilevile Mwaka wa Mawasiliano kati ya Watu wa China na Afrika.
Amesema Xinhua itachukua jukwaa hilo kama fursa ya kushirikiana na wenzake wa vyombo vya habari vya DRC ili kufafanua zaidi dira iliyowekwa na viongozi wa nchi zote mbili.
"Xinhua inalenga kueleza simulizi za kuvutia za ushirikiano wa pande mbili, kutafiti masuala ya kutazama siku za baadaye na ya kimkakati kuhusu maendeleo ya China na Afrika, na kuandaa shughuli za mawasiliano kama vile Jukwaa la Vyombo vya Habari na Taasisi za Washauri Bingwa la Nchi za Dunia ya Kusini," Fu ameongeza.
Naibu Waziri Mkuu wa DRC ambaye pia ni Waziri wa Uchumi wa Taifa Daniel Mukoko Samba amesema kwamba uhusiano wa muda mrefu kati ya China na DRC umekuwa ukiendelezwa kila mara kwa misingi ya ushirikiano na urafiki.
"Ushirikiano kati ya Afrika na China umetoa uungaji mkono muhimu kwa maendeleo ya bara la Afrika," ameongeza.
Patrick Muyaya, waziri wa mawasiliano na vyombo vya habari wa DRC na msemaji wa serikali, amesema jukwaa hilo linaashiria hatua mpya katika ushirikiano wa vyombo vya habari wa kati ya DRC na China.
Muyaya ametoa wito kwa pande zote mbili kuimarisha ushirikiano wa kitaasisi, kutafuta namna ya kuwa na matumizi ya teknolojia mpya kama vile mageuzi ya kidijitali na AI katika usambazaji wa habari, kufanya juhudi za pamoja kukabiliana na changamoto ya habari feki na kusukuma mbele kila mara uhusiano wa pande mbili.
Balozi wa China nchini DRC Zhao Bin amesema kuwa uhusiano wa sasa kati ya China na DRC uko katika hatua mpya ya kihistoria, na ujenzi wa mambo ya kisasa wa China utatoa fursa zaidi kwa maendeleo na ustawi wa DRC.
Jukwaa hilo lililoandaliwa kwa pamoja na Shirika la Habari la China, Xinhua na ACP, pia limeshirikisha maonyesho ya picha juu ya mafanikio ya ushirikiano kati ya China na DRC.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




