Lugha Nyingine
Mkoa wa Jiangsu, China watoa kipaumbele kwa roboti zenye umbo halisi kuwa sekta muhimu ya siku za baadaye (3)
![]() |
| Picha iliyopigwa Machi 10, 2026 ikionyesha kituo cha uvumbuzi wa roboti za AI mjini Suzhou, Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China. (Xinhua/Li Bo) |
Katika miaka ya hivi karibuni, Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China umetoa kipaumbele kwa roboti zenye umbo halisi kuwa sekta muhimu ya siku za baadaye. Vituo vya uvumbuzi na sehemu za kukusanya data na mafunzo kwa roboti hizo zenye umbo halisi za AI vimeanzishwa katika miji ikiwemo ya Nanjing, Suzhou na Wuxi.
Muungano wa viwanda vya roboti hizo zenye umbo halisi wa mkoa huo pia umeanzishwa, ukiwaleta pamoja washiriki karibu 300, wakiwemo wazalishaji, taasisi za utafiti, watumiaji wa mwisho na taasisi za fedha, ili kuunga mkono maendeleo ya sekta hiyo.
Katika sekta ya roboti za viwandani, mkoa huo wa Jiangsu ni nyumbani kwa kampuni ongozi kama vile Estun Automation na Inovance Group, na umeunda mfumo jumuishi unaohusisha roboti kamili na sehemu zake kuu. Mauzo ya nje ya roboti za viwandani kutoka mkoa huo yamedumisha ukuaji wa haraka.
Kwa maendeleo ya siku za baadaye, mkoa wa Jiangsu unapanga kujenga juu ya uungaji mkono wa kisera na majukwaa ya viwanda ili kuharakisha maendeleo ya kituo cha uvumbuzi wa roboti cha kitaifa, kusaidia kuleta matokeo ya utafiti kwenye mstari wa uzalishaji na kuingiza kasi mpya kwenye maendeleo yenye sifa bora ya uzalishaji bidhaa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




